Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UN News

Makala Maalum

Haki za binadamu Hali katika vituo vya rumande nchini Ufilipino, ambayo imeelezwa kuwa “si ya kibinadamu” na mmoja wa majaji wa mahakama ya juu nchini humo, inatarajiwa kuboreka kwa kasi wakati taifa hilo la Kusini Mashariki mwa Asia likielekea katika kupitisha sheria zinazozingatia haki za binadamu na utu wa wafungwa na kupendekeza kiwango cha chini cha matibabu katika vituo vyote vya rumande.

Habari Nyinginezo

Amani na Usalama Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa leo limeiitisha mjadala wa wazi kuhusu mgogoro unaoendelea Gaza, ambao unazidi kughubikwa na madhila makubwa yanayochangiwa na kuporomoka kabisa kwa ko mfumo wa sheria na utulivu na mfumo wa kibinadamu uko ukingoni kuporomoka kabisa.
Amani na Usalama Hali ya kibinadamu inaendelea kuwa mbaya Gaza huku leo mashirika ya kibinadamu ya Umoja wa  Mataifa yakiripoti kuendelea kwa mashambulizi yanayokatili maisha ya watu na kuathiri miundombinu ya raia kuanzia kwenye shule hadi vituo vya afya huku maelfu ya watu wakiendelea kukabiliwa na ukosefu wa huduma za msingi ikiwemo afya, makazi, maji  na  chakula kadri vita vinavyoendelea.