Mbolea itengenezwayo kwa taka za plastiki ni mkombozi maeneo ya ukame- Profesa Ruth
Kutana na Profesa Ruth Wanjau, mbobezi wa kemia katika Chuo Kikuu cha Kenyatta nchini Kenya, ambaye andiko lake la dhahania kuhusu mbolea itengenezwayo kwa kutumia taka za plastiki lilimkutanisha na wajasiriamali na wawekezaji kwenye Jukwaa la nne la kimataifa la uwekezaji kwa wajasiriamali, WEIF 2024 huko Manama nchini Bahrain, mwezi Mei mwaka huu.