Kuna mafanikio katika kampeni ya kukabiliana na hali ya kutokuwa na uraia: UNHCR
Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR) limetangaza kuwa zaidi ya watu nusu milioni ambao hawakuwa na uraia, wakinyimwa haki zao za kisheria, sasa wamepata uraia tangu kuanzishwa kwa kampeni ya #IBelong miaka kumi iliyopita. Kampeni hiyo, iliyolenga kumaliza tatizo la watu wasio na uraia, inakamilika mwaka huu.