Guterres atoa wito wa ulinzi kwa walinda amani baada ya IDF kukiuka msimamo wa UN Lebanon
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres leo Jumapili amesisitiza kwamba ulinzi na usalama wa wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa na mali za Umoja wa Mataifa lazima uhakikishwe, kufuatia uvunjaji wa makusudi wa sheria katika kituo cha Umoja wa Mataifa cha kulinda amani uliofanywa na magari ya kivita ya jeshi la Israel IDF kusini mwa Lebanon.