Watoto wanaokabiliwa na hatari kubwa zaidi ya unyanyasaji na unyonyaji wa kingono kutokana na matumizi mabaya ya teknolojia
Vitendo vya unyanyasaji na unyonyaji wa kingono dhidi ya watoto vimeongezeka katika mazingira ya kidijitali, huku zaidi ya watoto milioni 300 kwa mwaka wakikadiriwa kuwa waathiriwa wa vitendo hivyo mtandaoni, anasema Mama Fatima Singhateh ambaye ni Mjumbe Maalumu wa Umoja wa Mataifa kuhusu biashara na unyanyasaji wa kingono wa watoto.