Kugeuka sura
Yesu kugeuka sura ni sikukuu ya liturujia ya Ukristo inayoadhimisha fumbo la maisha ya Yesu linalosimuliwa katika Agano Jipya[1], hususan katika Injili Ndugu (Math 17:1–9, Mk 9:2-8, Lk 9:28–36) na katika 2 Pet 1:16–18[1].
Humo tunasoma kwamba Yesu Kristo aliongozana na wanafunzi wake watatu, Mtume Petro, Yakobo Mkubwa na mdogo wake Mtume Yohane, hadi mlima kwa lengo la kusali faraghani.
Huko usiku alianza kung'aa akatokewa na Musa na Eliya waliozungumza naye kuhusu kufariki kwake Yerusalemu.
Kubwa zaidi, Mungu Baba alimshuhudia kuwa Mwana wake mpenzi akawahimiza wanafunzi hao kumsikiliza.[1]
Hivyo Wakristo wanaona tukio hilo kama dhihirisho la Mwana pekee wa Mungu, mpendwa wa Baba wa milele, lililokusudiwa kuonyesha hadi miisho ya dunia kwamba hali duni ya binadamu aliyoitwaa imekombolewa kwa neema na kwamba jinsi ilivyoumbwa kwa mfano wa Mungu, sasa imeumbwa upya katika Kristo baada ya uharibifu uliosababishwa na Adamu [2].
Tukio linaheshimiwa hasa na Ukristo wa Mashariki na wamonaki wanaoliona mwaliko wa kutazama utukufu wa Mungu uliofichama katika malimwengu, kumbe kwa sala unadhihirika kwa macho ya imani.
Fumbo hilo linaadhimishwa kila mwaka kama sikukuu tarehe 6 Agosti[3]. Pia linazingatiwa katika Rozari kama tendo la nne la mwanga.
Picha
[hariri | hariri chanzo]-
Theofane Mgiriki, karne ya 15
-
Picha takatifu iliyochorwa na Andrey Ivanov, 1807
-
Giovanni Bellini, 1490 hivi
-
Pietro Perugino, 1500 hivi
Makanisa na monasteri
[hariri | hariri chanzo]-
Basilika la Kugeuka sura, Mlima Tabor
-
Basilika hiyohiyo tena
-
Shamba la Mungu la Wafransisko juu ya Mlima Tabor
Tanbihi
[hariri | hariri chanzo]- ↑ 1.0 1.1 1.2 Transfiguration by Dorothy A. Lee 2005 ISBN 978-0-8264-7595-4 pages 21-30
- ↑ https://www.santiebeati.it/dettaglio/21300
- ↑ Martyrologium Romanum
Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]- "The Transfiguration of Our Lord", Butler's Lives of the Saints
- . Catholic Encyclopedia. New York: Robert Appleton Company. 1913.
- The Mountain of the Transfiguration Ilihifadhiwa 12 Februari 2012 kwenye Wayback Machine. by Michele Piccirillo
- Pope Benedict XVI on Transfiguration of Jesus
- The Holy Transfiguration of our Lord God and Savior Jesus Christ Orthodox icon and synaxarion
Makala hii kuhusu dini ya Ukristo bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Kugeuka sura kama historia yake, matokeo au athari zake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |