Shilingi ya Tanzania
Mandhari
Shilingi ya Tanzania (kwa Kiingereza Tanzanian shilling; kifupi: TSh; code: TZS) ni fedha rasmi ya Tanzania. Imegawanyika katika senti (cents kwa Kiingereza) 100.
Shilingi ya Tanzania ilishika nafasi ya East African shilling tarehe 14 Juni 1966 at par.[1]
Kabla yake katika maeneo ya Tanzania ya sasa ziliwahi kutumika East African florin, East African rupee, Zanzibari rupee, Zanzibari riyal na German East African rupie.
Shilingi 100 zinaandikwa "100/=" au "100/-". Senti 50 zinaandikwa =/50 au -/50.
Tazama pia
[hariri | hariri chanzo]Tanbihi
[hariri | hariri chanzo]- ↑ Linzmayer, Owen (2012). "Tanzania". The Banknote Book. San Francisco, CA: www.BanknoteNews.com.
Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]Wikimedia Commons ina media kuhusu:
- Bank of Tanzania page on circulating banknotes Ilihifadhiwa 18 Januari 2013 kwenye Wayback Machine.