Misri ya Kale
Misri ya Kale ni ustaarabu uliokuwepo Africa, sambamba na mto Naili, kuanzia kwenye delta au mdomo wa Naili, kaskazini mwa Misri kwenda kusini hadi Jebel Barkal, penye maporomoko ya nne, wakati wa kupanuka kwake (Karne ya 15 KK).
Ustaarabu huu ulidumu kwa karibu milenia tatu, toka takribani mwaka 3000 KK hadi mwaka 30 KK nchi ilipovamiwa na Waroma na kuwa sehemu ya Dola la Roma.
Uti wa mgongo wa Misri ya Kale ulikuwa mto Naili. Sehemu kubwa ya nchi ni jangwa lakini umwagiliaji wa mashamba kwa njia ya maji ya mto ulileta mazao mazuri yaliyolisha watu wengi. Mahitaji ya kupanga na kutunza mifereji pamoja na mitambo ya umwagiliaji na kusimamia ugawaji wa maji yalisaidia kutokea kwa vyanzo vya hisabati na mwandiko. Mwandiko wa Misri ulikuwa hiroglifi zilizokuwa aina ya mwandishi wa picha.
Dini ya Misri ilitarajia maisha baada ya kifo ambayo yanapaswa kuandaliwa na watu wakati wa maisha huu. Wafalme waliokuwa na cheo cha farao walipewa makaburi makubwa sana na piramidi ni kati ya makaburi makubwa kabisa duniani. Duniania ya Kale ya Misri; Nubia Kush Napata Thebes Memphis Giza Gezira Saqara Luxor Aswan Kom Ombo Sinai St.Catharines Abu Simbel
Kigezo:Link FA Kigezo:Link FA Kigezo:Link FA Kigezo:Link FA Kigezo:Link FA