Jicho Quotes

Quotes tagged as "jicho" Showing 1-2 of 2
Enock Maregesi
“Yesu alipokuwa msalabani watu wengi walimzunguka. Askari wa Kirumi aliyekuwa na chongo, na mkuki, alikuwa na jukumu la kumtesa Yesu hadi kufa kwa amri ya Pilato. Yesu alipolia kwa sauti kuu, “Eloi, Eloi, lama sabakthani?”, yule askari alikurupuka na kumwendea Yesu. Lakini Yesu alishakata roho. Kuthibitisha kama Yesu alishakata roho, askari alimchoma Yesu mkuki kwenye mbavu kwa nguvu zake zote. Mkuki huo ukamtoboa Yesu hadi upande wa pili, ukatoboa hata moyo wake. Askari alipochomoa mkuki, damu na maji viliruka na kupiga jicho lake bovu. Papo hapo askari akapona na kuona vizuri. Alipoona kweli amepona na kuona vizuri, askari alipiga kelele, alipiga magoti na kuomba Mungu amsamehe dhambi zake. Msamaha una nguvu kuliko dhambi. Askari huyo atakwenda mbinguni. Haijalishi umechukia watu kiasi gani. Haijalishi umetesa watu kiasi gani. Haijalishi umeua watu kiasi gani. Haijalishi umetenda dhambi kiasi gani. Mungu anachotaka kutoka kwako, tubu.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Jicho ni kiungo cha ajabu zaidi kuliko viungo vyote katika mwili wa mwanadamu baada ya ubongo. Jicho moja linatengenezwa na viungo vidogovidogo zaidi ya milioni mbili, vinavyofanya kazi kwa pamoja bila kukosea. Macho yana nguvu ya ajabu. Huu ni wito kwa akina mama wanaonyonyesha: Usizungumze maneno mabaya mtoto wako mchanga anapokuangalia machoni wakati ananyonya ziwa lako. Neno lolote utakalomwambia, zuri au baya, pamoja na kwamba amekuwa akisikia sauti yako kwa miezi kadhaa akiwa tumboni, litajirekodi katika akili yake isiyotambua bila wewe au yeye mwenyewe kujua. Neno hilo litakuja kumuathiri baadaye atakapokuwa mkubwa. Atakapopevuka, atakapokuwa na uwezo wa kupambanua mambo, atakuwa anaota na kuwaza kile ambacho ulikuwa ukimwambia alipokuwa tumboni; na alipokuwa akinyonya na kukukodolea macho.”
Enock Maregesi