Nenda kwa yaliyomo

Youssou N'Dour

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Youssou N'Dour
Taarifa za awali
Jina la kuzaliwaYoussou N'Dour
Amezaliwa1 Oktoba 1959 (1959-10-01) (umri 65)
Dakar, Senegal
Kazi yakeMwimbaji, mtunzi wa nyimbo, mwanamuziki
AlaSauti, gitaa
Miaka ya kazi1979 - sasa
Ameshirikiana naSuper Étoile de Dakar
WavutiOfficial website

Youssou N'Dour (amezaliwa 1 Oktoba, 1959) ni mwimbaji, mtunzi wa nyimbo, na mwanamuziki maarufu kutoka Senegal. Anajulikana kimataifa kwa sauti yake ya kipekee na mchango wake katika muziki wa Afrika. Baadhi ya nyimbo zake maarufu ni pamoja na 7 Seconds (1994) - ft. Neneh Cherry, Birima (2000), Nelson Mandela (1986), Ob-La-Di, Ob-La-Da (1995) (cover ya Beatles), Set (1990), Shaking the Tree (1990) - ft. Peter Gabriel, New Africa (1989), Medina (1997), My Hope is in You (1994) na Africa Dream Again (1996).

Muziki na maisha

[hariri | hariri chanzo]

Youssou N'Dour alianza kufanya muziki katika miaka ya 1970 akiwa kijana. Alianzisha bendi yake ya kwanza, Super Étoile de Dakar, ambayo ilichochea ukuaji wa aina ya muziki wa "Mbalax." Muziki ambao ni mchanganyiko wa muziki wa asili wa Senegal na muziki wa kisasa.

Baadaye, N'Dour alipata umaarufu ulimwenguni kwa kipawa chake cha sauti yake ya kipekee. Pia kuweza kuchanganya mitindo mbalimbali ya muziki. Aliendelea kutoa albamu nyingi zilizofanikiwa, ambazo zilimfanya awe mmoja wa wanamuziki mashuhuri kutoka Afrika.

Katika safari yake ya kumuziki, amefanikiwa kujishindia tuzo mbalilimbali. Ikiwa ni pamoja na Grammy kwa albamu zake za "Egypt" na "Rokku Mi Rokka," ambazo zilikuwa na athari kubwa kwa tasnia ya muziki wa dunia. Pia amekuwa balozi wa utamaduni wa Senegal ulimwenguni kote.

Mbali na muziki, Youssou N'Dour amewahi kujihusisha sana na siasa na shughuli za kijamii nchini Senegal. Alijitupa katika kinyang'nyiro cha kuwania urais wa Senegal mwaka 2012, akigombea dhidi ya rais wa wakati huo, Abdoulaye Wade.

Diskografia

[hariri | hariri chanzo]

Baadhi ya albamu maarufu za Youssou N'Dour ni pamoja na:

  • Immigrés (1984)
  • The Lion (1989)
  • Eyes Open (1992)
  • Egypt (2004)
  • Rokku Mi Rokka (2007)
  1. *Biography of Youssou N'Dour* - BBC News
  2. *Youssou N'Dour: The Voice of Senegal* - CNN
  3. *Official Website of Youssou N'Dour Ilihifadhiwa 21 Februari 2024 kwenye Wayback Machine.*

Viungo vya Nje

[hariri | hariri chanzo]
Makala hii kuhusu mwanamuziki fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Youssou N'Dour kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.


Makala hii ni sehemu ya mradi wa kuboresha Wikipedia na Wikamusi ya Kiswahili. Unaweza kusaidia kuihariri na kuongeza habari.