Wikipedia ya Kinorwei
Kuna matoleo mawili ya Wikipedia kwa lugha ya Kinorwei: moja kwa ajili ya makala zinazoandikwa kwa Bokmål au Riksmål, na moja kwa ajili ya makala zinazoandikwa kwa lugha ya Nynorsk. Tovuti ya kwanza, yaani, Wikipedia halisi ya Kinorwei, ilianzishwa mnamo tar. 26 Novemba 2001, na hiyo ilikuwa ikiruhusu makala ziandikwe kwenye kiwango cha Kinorwei cha kawaida.
Wikipedia ya Kinorwei cha Nynorsk ilianzishwa mnamo 31 Julai 2004 na ikakua haraka sana. Kwa kufuatia kula zilizopigwa mnamo mwaka wa 2005, ukurasa wa mwanzo wa Kinorwei uikuwa unataja lugha zote mbili, yaani, Bokmål na Riksmål.
Mnamo mwezi wa Februari ya mwaka wa 2007, toleo la Bokmål/Riksmål ilimekuwa na zaidi ya makala 100,000 na toleo la Nynorsk likawa na zaisi ya makala 20,000. Mnamo Februari 2006, ikawa Wikipedia ya kumi na tatu kuwa na makala zaidi ya 50,000, na baada ya mwaka mmoja ikawa ya kumi na nne kufikisha makala 100,000.
Hata hivyo, ikaja kupitwa mnamo Aprili 2006 na Wikipedia ya Kifini na kuifanya iwe ya kumi na nne kwa hesabu ya wingi wa makala.[1]
Tazama pia
[hariri | hariri chanzo]Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ [1]. As of 16 Februari 2009, the Bokmål/Riksmål contains more than 200,000 articles, while the Nynorsk version contains over 45,000
Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]- Norwegian Wikipedia (Bokmål and Riksmål)
- Norwegian Wikipedia (Nynorsk)
- Meta: Skanwiki
- Wikimedia Norge, interim website on meta
Makala hii kuhusu mambo ya elimu bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Wikipedia ya Kinorwei kama historia yake, uenezi au maendeleo yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |