Nenda kwa yaliyomo

Wema Sepetu

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Wema Abraham Sepetu (alizaliwa 28 Septemba 1988)[1] ni mwanamitindo, mjasiriamali na mwigizaji kutoka nchini Tanzania.

Aliwahi kuwa Miss Tanzania kwa mwaka wa 2006. Aliiwakilisha Tanzania katika Miss Dunia 2006[2], ambayo ilifanyika nchini Poland. Baadaye alikua mwigizaji nchini Tanzania.[3]

Maisha ya awali, elimu, na sanaa

[hariri | hariri chanzo]

Wema ni mtoto wa mwisho katika familia ya watoto wanne wa mwanadiplomasia Abraham Sepetu. Alianza elimu ya msingi na hadi sekondari amesomea katika shule moja tu iitwayo "Academic International" iliyopo maeneo ya Mikocheni, jijini Dar es Salaam. Pamoja na yote hayo, binti huyu amelelewa na kuishi kama mtu wa Magharibi. Baadaye alijiunga na Chuo Kikuu cha Ubunifu wa Teknolojia cha Limkokwing nchini Malaysia kusoma kozi ya biashara za kimataifa ambayo alisoma kwa mwaka mmoja, kisha akakatisha masomo ili kuendelea na uigizaji.

Kipaji zaidi cha Wema kiligundulika katika sanaa ya filamu, ambapo alifanikiwa kucheza vema kabisa katika filamu A Point of No Return akishirikiana na mchezaji filamu maarufu wa Kitanzania Steven Kanumba.

Wema alivishwa pete ya uchumba na msanii maarufu wa Bongo Flava Diamond Platnumz, lakini kwa sasa wameshaachana.

Pia Wema amekuwa akijulikana kwa kuwa na sauti ndogondogo.

Miss Tanzania 2006 na Miss World 2006

[hariri | hariri chanzo]

Baada ya kushinda taji la Miss Tanzania mnamo 2006, Wema alisafiri kwenda Warsaw, Poland kushindana katika kinyanganyiro cha Miss World 2006, hata hivyo hakufanikiwa kuingia katika kumi na saba bora.

Uigizaji

[hariri | hariri chanzo]
  • Aliingizwa kwenye tasnia ya sinema na marehemu Steven Kanumba wakati wa uchumba wao, alifanya filamu yake ya kwanza kwa jina la Apoint of no return akiigiza kama Dina akiwa mhusika mkuu pamoja na Steven Kanumba, aliigiza kama binti mdogo ambaye analazimishwa na familia yake kuolewa na Lameck (Steven Kanumba) aliekuwa mchawi na ambaye sio chaguo lake. Baadaye alionekana kwenye sinema nyingi kama vile Family Tears, Red Valentine,White Maria ambazo zilimfanya kuwa mmoja wa waigizaji maarufu nchini Tanzania. Ameonekana katika filamu zaidi ya 20.
  • Mnamo mwaka 2011 alitengeneza sinema iitwayo Superstar, filamu ambayo inaelezea maisha yake ya kimahusiano na mwanamuziki Diamond Platnumz.[4] Sinema hiyo ilizinduliwa mnamo mwaka 2012 katika Hoteli ya Kilimanjaro Hyatt Regency jijini Dar Es salaam na ilisifiwa na watu wengi akiwemo Omotola Jalade Ekeinde kutoka Nigeria ambaye alikuwa mgeni wa heshima.[5] Lakini sinema haikuingia sokoni hadi leo na Wema alisema kuwa bado anatafuta msambazaji bora ambaye anaweza kumlipa kulinganisha na gharama zake za uzalishaji kwani alisema kwamba wasambazaji wengi wameahidi pesa kidogo ikilinganishwa na kile alichowekeza.[6] Baada ya hapo alionekana kwenye sinema kama Basilisa,It was not me,House boy, Madame kati ya nyingi.
  • Mnamo mwaka 2014 alishirikiana na Van Vicker kutoka nchini Ghana kutengeneza sinema iitwayo Day After Death wakiwa kama waigizaji wakuu.[7] Filamu hiyo ilipangwa kutolewa mnamo mwaka 2015,[8]lakini kutokana na ucheleweshaji haijaingia sokoni hadi leo, mbali na D.A.D kutoachiliwa. Kwa bahati nzuri wakati wa kusherehekea siku yake ya kuzaliwa ya miaka 30 alifanya uzinduzi wa sinema ya DAD na kuifanya kuwa sinema pendwa zaidi. Wema alionekana katika sinema zingine kutoka 2015-2016 kama vile Family, Mapenzi Yamerogwa and Chungu Cha Tatu kati ya nyingi.
  • Mnamo mwaka 2017 alirejea na filamu yake kwa jina la Heaven Sent, ambayo aliitengeneza na kuwa mhusika mwongozaji ambayo pia alikuwa na Salim Ahmed (Gabo) kama mhusika mkuu, uzinduzi huo ulifanyika Century Cinemax Mlimani City jijini Dar Es salaam nchini Tanzania.[9] sinema iliuzwa kupitia programu yake ya rununu (simu) Wema App. Filamu hii iliteuliwa katika vipengele saba (7) kwenye tukio la Sinema Zetu International Film Festival Awards 2018, pamoja na muigizaji Bora wa kike na Filamu Bora ya Kipindi,[10] ambapo Wema alishinda Mwigizaji Bora wa kike na sinema ilishinda Chaguo la Watu.

Endeless Fame Production

[hariri | hariri chanzo]

Mnamo mwaka 2013 alizindua kampuni yake kwa jina la Endless Fame Production.[11] Shirika hilo linahusika na utengenezaji wa sinema na Usimamizi wa wasanii, wameweza kusimamia baddhi ya wanamuziki wa Kitanzania kama vile Mirror na Ally Luna. Shirika hilo limetengeneza sinema kama vile Supestar, Unexpected, Day After Death, Family, and Heaven Sent.

Baadhi ya filamu za Wema

[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]
  1. PeoplePill. "Wema Sepetu: Tanzanian beauty pageant winner (1988-) | Biography, Facts, Career, Wiki, Life". PeoplePill (kwa American English). Iliwekwa mnamo 2020-08-22.
  2. "Miss World 2006 contestants Miss Tanzania: Wema Isaac Sepetu , Miss..." Getty Images (kwa American English). Iliwekwa mnamo 2020-03-31.
  3. Zindzy Gracia (2018-08-21). "Wema Sepetu biography: age, boyfriend, child and latest photos". Tuko.co.ke - Kenya news. (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2020-03-31.
  4. "PICHA ZA WEMA SEPETU AKIWA ANAANDAA MOVIE YAKE MPYA YA SUPERSTAR | Teen blog swaggz". PICHA ZA WEMA SEPETU AKIWA ANAANDAA MOVIE YAKE MPYA YA SUPERSTAR | Teen blog swaggz. 2013-02-13. Iliwekwa mnamo 2020-04-01.
  5. "Red Carpet Photos: Wema Sepetu's Glittered Night Event". Bongo5.com (kwa American English). 2012-06-25. Iliwekwa mnamo 2020-04-01.
  6. Unknown (2014-11-13). "SWP: Superstar Ya Wema Sepetu Kuingia Sokoni Muda Si Mrefu". SWP. Iliwekwa mnamo 2020-04-01.
  7. "Picha: Wema Sepetu na Van Vicker wafanya movie Ghana, inaitwa 'Day After Death'". Bongo5.com (kwa American English). 2014-12-10. Iliwekwa mnamo 2020-04-01.
  8. "Filamu ya Van Vicker na Wema Sepetu 'Day After Death' kuzinduliwa September, Dar (Video)". Bongo5.com (kwa American English). 2015-05-25. Iliwekwa mnamo 2020-04-01.
  9. "Wema Sepetu Azindua Filamu Yake Kwa Kishindo Mlimani City, Dar (Video)". Global Publishers. 2017-08-27. Iliwekwa mnamo 2020-04-01.
  10. "SZIFF - International Film Festival Tanzania". sziff.co.tz. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2020-09-22. Iliwekwa mnamo 2020-04-01.
  11. MP. "What Wema Sepetu wore for her Office Launch" (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2020-04-01.
Makala hii kuhusu mwigizaji filamu fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Wema Sepetu kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.