Usimamizi
Usimamizi (kutoka kitenzi kusimamia; kwa Kiingereza "management"[1]) katika biashara na katika shughuli ya kuwapanga binadamu ni kitendo cha kuwaweka watu pamoja ili kutimiza malengo na madhumuni yatakikanayo. Usimamizi unajumuisha mipango, kuandaa, kuajiri wafanyakazi, kuongoza na kudhibiti shirika (kundi la mtu mmoja au zaidi au wahusika) au juhudi kwa madhumuni ya kufanikisha lengo. Kugawanya rasilimali kunajumuisha kupelekwa na kutumika kwa rasilimali watu, fedha, teknolojia na maliasili.
Usimamizi unaweza pia kumrejelea mtu au watu wanaotenda tendo au matendo ya usimamizi.
Ufafanuzi
[hariri | hariri chanzo]Baadhi ya ufafanuzi wa usimamizi ni:
- Mpango na uratibu wa shughuli ya kibiashara kulingana na sera fulani na katika kufanikisha malengo yaliyofafanuliwa vyema. Usimamizi unahusishwa katika vito vya uzalishaji kama vile mashine, vifaa na pesa. Kulingana na gwiji wa usimamizi Peter Drucker (1909-2005), kazi ya msingi ya usimamizi ni mardufu: masoko na uvumbuzi.
- Wakurugenzi na mameneja ambao wana uwezo na wajibu wa kufanya maamuzi ya kusimamia biashara. Kama nidhamu, usimamizi unajumuisha shughuli zinazohusiana za kubuni sera ya shirika na kuandaa, kupanga, kudhibiti, na kuelekeza rasilimali za kampuni ili kufikia malengo ya sera. Upana wa usimamizi unaweza kuwa kati ya mtu mmoja katika kampuni ndogo hadi mamia au maelfu ya wakurugenzi katika makampuni ya kimataifa. Katika makampuni makubwa, bodi ya wakurugenzi hubuni sera ambayo inatekelezwa na afisa mtendaji mkuu.
Nadharia wigo
[hariri | hariri chanzo]Mary Parker Follett (1868-1933), ambaye aliandika juu ya mada hii mapema katika karne ya 20, aliufafanua usimamizi kama "sanaa ya kufanya vitu vifanywe kupitia kwa watu". Pia aliuelezea usimamizi kama falsafa. [2]
Mtu anaweza kufikiria pia usimamizi kiutendaji, kama hatua ya kupima kiasi mara kwa mara na kurekebisha baadhi ya mipango ya awali; au kama hatua zilizochukuliwa kufikia lengo la mtu. Hii inatumika hata katika hali ambapo kupanga hakufanyiki. Kufuatia mtazamo huu, Mfaransa Henri Fayol [3] anauchukulia usimamizi kuwa na vipengele saba:
- kupanga
- kuandaa
- kuongoza
- kuratibu
- kudhibiti
- kuweka wafanyakazi
- kuhamasisha
Baadhi ya watu, hata hivyo, huona ufafanuzi huu, ingawa ni muhimu, kuwa finyu mno. Msemo "usimamizi ni kile ambacho mameneja hufanya" hutokea sana, na kupendekeza ugumu wa kuufafanua usimamizi, asili ya kubadilika badilika ya fasili, na uhusiano wa matendo ya usimamizi na kuwepo kwa viwango au madarasa ya usimamizi.
Tabia moja ya fikra kuhusu usimamizi, inauchukulia kama sawa na "utawala wa biashara " na hivyo haihusishi usimamizi katika maeneo nje ya biashara, kama kwa mfano katika kutoa misaada na katika sekta ya umma. Bayana zaidi, hata hivyo, kila shirika lazima lisimamie kazi yake, watu, taratibu, teknolojia, nk ili kuendeleza kabisa ufanisi wake. Hata hivyo, watu wengi hurejea idara za vyuo vikuu ambavyo hufundisha usimamizi kama "shule za kibiashara." Baadhi ya taasisi (kama Shule ya Biashara ya Harvard) hutumia jina hilo wakati nyingine (kama vile Shule ya Usimizi ya Yale) hutumia neno jumuishi zaidi "usimamizi."
Wazungumzaji wa lugha ya Kiingereza pia huweza kutumia neno "usimamizi" au "kusimamia" kama neno shirkishi linaloeleza mameneja wa shirika, kwa mfano wa Kampuni. Kihistoria matumizi haya ya neno hili, mara nyingi lilitofautishwa na neno "leba" likimaanisha wale wanaosimamiwa.
Asili ya kazi ya usimamizi
[hariri | hariri chanzo]Katika kazi za faida, kazi ya msingi ya usimamizi ni kuridhisha makundi mbalimbali ya washikadau. Hii kwa kawaida inahusisha kutengeza faida (kwa wanahisa), kujenga vitu vya thamani kwa gharama ya chini (kwa wateja), na kutoa fursa ya ajira yenye faida (kwa wafanyakazi). Katika usimamizi usio wa faida, kuongeza umuhimu wa kuhifadhi imani ya wafadhili. Katika mifano mingi ya usimamizi / utawala, wanahisa hupigia kura bodi ya wakurugenzi na kisha bodi inaajiri usimamizi mkuu. Baadhi ya mashirika yamefanya majaribio na njia nyingine (kama mfanyakazi-kupiga kura) ya kuchagua au kubadilisha watawala; lakini hii hutokea tu mara chache sana.
Katika sekta ya umma ya nchi zilizopangwa kama demokrasia ya uwakilishi, wapigaji kura huwapigia kura wanasiasa kwenda afisi ya umma. Wanasiasa hao huwaajiri mameneja na wasimizi wengi, na katika baadhi ya nchi kama Marekani wateule wa kisiasa hupoteza ajira kwa sababu ya uchaguzi wa rais mpya / gavana / meya.
Maendeleo ya kihistoria
[hariri | hariri chanzo]Matatizo hutokea katika kufuatilia historia ya usimamizi. Baadhi huuona (kwa ufafanuzi) kama njia chelewa ya kisasa (kwa maana ya usasa uliochelewa) ya fikra. Kwa maneno hayo haiwezi kuwa kabla ya historia ya kisasa, ni watangulizi tu (kama wangojezi). Wengine, hata hivyo, huona dhana ya usimamizi kwa wafanyabiashara wa Kisumeri na wajenzi wa piramidi za Misri ya kale. Wamiliki watumwa kwa karne walikabiliwa na matatizo ya kutumia / kuwahamasisha wafanyakazi wa kutegemwa lakini wakati mwingine wasiojiskia au wasiotaka, lakini mengi ya makampuni kabla ya enzi ya viwanda, kutokana na udogo wao, hayakuona umuhimu wa kukabili maswala ya usimizi kimfumo. Hata hivyo, uvumbuzi kama vile kuenea kwa nambari za Kiarabu (karne ya 5 hadi ya 15) na kuanzishwa kwa kanuni ya mwingilio mara mbili kwa vitabu vya hesabu (1494) kulichangia vyombo vya kutathmini, kupanga na kudhibiti.
Kutokana na ukubwa wa shughuli za kibiashara na ukosefu wa uhifadhi kumbukumbu na kurekodi kwa kutumia mashine kabla ya mapinduzi ya kiviwanda, ilieleweka kwa wamiliki wengi wa makampuni katika nyakati hizo kuendesha shughuli za usimamizi, wao wenyewe. Lakini kutokana na kuongezeka kwa ukubwa na utata wa mashirika, mgawanyiko kati ya wamiliki (watu binafsi, falme za kiviwanda au makundi ya wanahisa) na mameneja wa siku-hadi-siku (wataalamu wa kujitegemea katika kupanga na kudhibiti) polepole ikawa ni kawaida.
Maandiko ya mapema
[hariri | hariri chanzo]Wakati usimamizi imekuwepo sasa kwa milenia kadhaa, waandishi kadhaa waliumba kinyume cha matendo ambayo yalisaidia katika nadharia ya usimamizi wa kisasa. [4]
The Art of War - Sanaa ya Vita chake Sun Tzu
[hariri | hariri chanzo]Kilichoandikwa na jenerali wa Kichina Sun Tzu katika karne ya 6 KK, Sanaa ya Vita ni kitabu cha mkakati wa kijeshi ambacho, kwa madhumuni ya usimamizi, kinapendekeza kuwa kufahamu na kutenda kwa kuzingatia uwezo na udhaifu wa shirika la meneja na wa adui.[4]
The Prince - Mtawala chake Niccolo Machiavelli
[hariri | hariri chanzo]Kwa kuamini kwamba watu walipewa motisha kwa kujitafutia riba, Niccolo Machiavelli aliandika The Prince mwaka 1513 kama ushauri kwa uongozi wa Florence, huko Italia. [5] Machiavelli alipendekeza kwamba viongozi watumie hofu-lakini si chuki-kudumisha udhibiti.
The Wealth of Nations - Utajiri wa Mataifa chake Adam Smith
[hariri | hariri chanzo]Kiliandikwa mwaka wa 1776 na Adam Smith, mwanafalsafa wa kimaadili Mskoti, The wealth of nations, kinalenga uratibu mzuri wa kazi kupitia Umaalumu wa kazi. [5] Smith alielezea jinsi mabadiliko katika michakato ingeweza kuimarisha tija katika utengezaji wa pini. Wakati watu binafsi wangeweza kuzalisha pini 200 kwa siku, Smith alitathmini hatua zilizohusika katika utengenezaji na, pamoja na wataalam 10, kuwezeshwa uzalishaji wa pini 48,000 kwa siku. [5]
Karne ya 19
[hariri | hariri chanzo]Wanauchumi wa wakati huo kama Adam Smith (1723 - 1790) na John Stuart Mill (1806 - 1873) walitoa nadharia ya msingi kwa masuala ya mgao wa rasilimali, uzalishaji na bei. Kuhusu hayo, wavumbuzi kama Eli Whitney (1765 - 1825), James Watt (1736 - 1819), na Mathew Boulton (1728 - 1809) waliendeleza vipengele vya uzalishaji wa kiufundi kama vile kuweka viwango, taratibu za kudhibiti ubora, kuhasibu gharama, uwezo wa kubadilishana kwa sehemu, na kupanga kazi. Mengi ya masuala hayo ya usimamizi yalikuwepo katika sekta ya uchumi uliotegemea utumwa kabla ya 1861 huko Marekani. Mazingira haya yaliona watu milioni 4, kama vile matumizi ya kisasa yasemayo, "kusimamiwa" kwa faida uzalishaji mwingi.
Kwa karne ya 19, wanauchumi wa pembeni Alfred Marshall (1842-1924), Leon Walras (1834-1910), na wengine walianzisha safu mpya ya utata kwa msingi wa nadharia ya usimamizi. Joseph Wharton alitoa msingi wa kwanza wa ngazi kozi katika usimamizi mnamo 1881.
Karne ya 20
[hariri | hariri chanzo]Kufikia mwaka 1900 tunanaona mameneja wakijaribu kuweka nadharia zao juu ya kile wao walikiona kama msingi wa kisayansi kabisa (tazama shauku kwa Usayansi kwa upungufu wa imani hii). Mifano ni pamoja na Science of management -S ayansi ya usimamizi chake Henry R. Towne katika miaka ya 1890, The principles of Scientific Management - Kanuni za kisayansi za Usimamizi cha (1911), chake Frederick Taylor Winslow, Applied motion study (1917) chao Frank na Lillian Gilbreth, na chati (miaka ya 1910) chake Henry Yale Gantt. J. Duncan aliandika kitabu cha kiada cha kwanza cha usimamizi cha chuo mwaka wa 1911. Mnamo 1912 Yoichi Ueno alianzisha sera za Taylor za usimamizi huko Ujapani na akawa mshauri wa kwanza wa "Kijapani wa mitindo ya usimamizi". Mwanawe Ichiro Ueno alitanguliza uhakikishaji usawa katika Ujapani.
Nadharia pana ya kwanza ya usimamizi ilitokeza karibia 1920. Shule ya Kibiashara ya Harvard ilizindua shahada ya Masta ya Usimamizi wa Biashara (MBA) mnamo 1921. Watu kama Henri Fayol (1841 - 1925) na Alexander Church alielezea matawi mbalimbali ya usimamizi na uhusiano kati yao. Mapema katika karne ya 20, watu kama Ordway Tead (1891-1973), Walter Scott na J. Mooney walitumia kanuni za saikolojia katika uongozi, wakati waandishi wengine, kama vile Elton Mayo (1880-1949), Mary Parker Follett (1868 - 1933), Chester Barnard (1886-1961), Max Weber (1864-1920), Rensis Likert (1903 - 1981), na Chris Argyris (1923 -) waliutama uzushi wa usimamizi kutoka mtazamo wa kisoshiolojia.
Peter Drucker (1909 - 2005) aliandika moja ya vitabu vya mapema juu ya kutumia usimamizi: Dhana ya Shirika "Concept of the Corporation" (kilichochapishwa mwaka wa 1946). Ilitokana na Alfred Sloan (mwenyekiti wa General Motors hadi 1956) kuanzisha utafiti wa shirika. Drucker aliendelea mbele na kuandika vitabu 39, vingi kwenye suala hili.
H. Dodge, Ronald Fisher (1890 - 1962), na Thornton C. Fry walianzisha mbinu za kutumia takwimu katika utafiti wa usimamizi. Katika miaka ya 1940, Patrick Blackett aliunganisha takwimu hizi za nadharia kwa nadharia ndogo ya kibiashara na kuzua sayansi ya utafiti wa oparesheni. Operations utafiti, wakati mwingine hujulikana kama "usimamizi sayansi" (lakini tofauti kutoka usimamizi wa kisayansi wake Taylor, majaribio ya kuchukua mbinu za kisayansi za usimamizi kutatua matatizo, hasa katika maeneo ya vifaa na utendaji.
Baadhi ya maendeleo zaidi ni pamoja na nadharia ya vipingamizi, usimamizi kwa madhumuni, uhandisi upya, Six Sigma na nadharia zinazoendeshwa na teknolojia ya habari kama programu inayoundwa kwa mfumo wa kubadilika, na nadharia za usimamizi wa kundi kama Ngazi ya Cog.
Kutambuliwa kwa mameneja kama darasa kuliimarika katika karne ya 20 na kuwapa walionekana kuwa watekelezaji wa sanaa / sayansi ya kusimamia kiasi fulani cha ufahari, hivyo njia ilifunguka kwa mawazo maarufu yamifumo ya usimamizi kuuzwa. Katika muktadha huu mitindo mingi ya usimamizi inaweza kuwa ilikuwa zaidi inahusiana na saikolojia ya pop kuliko nadharia ya usimamizi wa kisayansi.
Kuelekea mwisho wa karne ya 20, usimamizi wa biashara ulikuja kujumisha matawi sita tofauti, yaani:
- Usimamizi wa rasilimali watu
- Usimamizi wa operesheni au usimamizi wa uzalishaji
- Usimamizi wa Kimkakati
- Usimamizi uuzaji
- Usimamizi wa kifedha
- Teknolojia ya habari inayowajibikia usimamizi wa mifumo ya usimamizi wa habari
Karne 21
[hariri | hariri chanzo]Katika karne ya 21 waangalizi wanakuta kuwa ni vigumu kuugawanya usimamizi kwa makundi kwa njia hii. Michakato zaidi kwa wakati huo huo inahusisha makundi kadhaa. Badala yake, mtu hufikiria katika misingi ya michakato mbalimbali, majukumu, na vitu chini ya usimamizi.
Matawi ya usimamizi wa nadharia pia ipo inayohusiana na mashirika yasiyo ya kibiashara na kwa serikali: kama vile utawala wa umma, menejimenti ya umma na usimamizi wa elimu. Aidha, mipango ya usimamizi wa unaohusiana na mashirika ya kijamii imetoa pia mipango katika usimamizi wa mashirika yasiyo ya kibiashara na ujasiriamali wa kijamii.
Kumbuka kwamba mengi ya mawazo ya usimamizi yameshambuliwa na makundi ya [[maadili ya biashara], masomo ya utafiti wa usimamizi na uanaharakati wa kupambana na ushirika.
Kwa sabau hiyo, demokrasia mahali pa kazi imezidi kuwa kawaida, na kuzidi kutetewa, katika baadhi ya maeneo shughuli zote za usimamizi zimesambazwa miongoni mwa wafanyakazi, kila mmoja ambaye anachukua sehemu ya kazi. Hata hivyo, mifano hii inatangulia masuala ya kisiasa ya sasa, na huweza kutokea kiasili zaidi kuliko ngazi ya Kiamri. Usimamizi wote kwa kiwango fulani lazima uzingatie misingi ya kidemokrasia kwani kwa kipindi kirefu ni lazima wafanyakazi wauunge mkono usimamizi kwa kiwango kikubwa; vinginevyo wao huondoka kutafuta kazi nyingine, au kugoma. Licha ya kuelekea kwa mfumo wa demokrasia katika sehemu za kazi, muundo wa amri-na-udhibiti wa mashirika ni kawaida na unaendelea kuwa ni muundo wa kawaida wa mashirika. Hakika tabia ya amri-na-kudhibiti inaweza kuonekana kwa jinsi ambayo wafanyakazi kuachishwa kazi hivi karibuni kumetekelezwa, safu ya usimamizi imeathiriwa kidogo sana ukilinganisha na wafanyakazi wa kiwango cha chini katika mashirika. Katika baadhi ya matukio, usimamizi umajizawadia bahkshishi wakati ambapo wafanyakazi wa kiwango cha chini wamekuwa wakiachishwa kazi. [6]
Miktadha ya usimamizi
[hariri | hariri chanzo]Shughuli za msingi za usimamizi
[hariri | hariri chanzo]Usimamizi hufanya kazi kupitia shughuli mbalimbali, mara nyingi zimegawanywa kama kupanga, kuandaa, kuongoza / kuhamasisha, na kudhibiti.
- Mipango: Kuamua yale yanayohitajika kufanyika usoni (leo, wiki ijayo, mwezi ujao, mwaka kesho, miaka 5 ijayo, nk) na kutoa mipango ya utendaji kazi.
- Kuandaa: (Utekelezaji) kutumia kikamilifu rasilimali zinazohitajika kuwezesha kufaulu kwa matekelezo ya mipango.
- Utumishi: Kuchunguza kazi, kuajiri, na kuwaajiri watu kwa ajira mwafaka.
- Uongozi: kuamua nini kinafaa kufanywa katika hali fulani na kuwafanya watu kufanya hivyo.
- Kudhibiti: Ufuatiliaji, kuangalia mafanikio dhidi ya mipango, ambayo inawezahitaji mabadiliko kutegemea matokeo.
- Kuhamasisha: mchakato wa kumchochea mtu binafsi achukue hatua ambayo itatimiza lengo..
Kuunda sera za kibiashara
[hariri | hariri chanzo]- Misheni ndio kusudi lake dhahiri sana - ambayo inaweza kuwa, kwa mfano, kutengeneza sabuni.
- Maono ya biashara huangazia matarajio yake huelezea mwelekeo au nia ya inapoelekea.
- Malengo ya biashara yanarejelea matokeo au kazi ambayo shughuli fulani inalenga.
- Sera ya biashara ni mwongozo unaoelezea sheria, kanuni na malengo, na inaweza kutumika katika maamuzi ya mameneja. Ni lazima iwe rahisi kufasiriwa na kueleweka kwa urahisi na wafanyakazi wote.
- Mkakati wa biashara unahusu mpango wa utekelezaji ulioratibishwa utakaofuatwa, pia rasilimali zitakazotumika, kufanikisha maono na malengo yake ya muda mrefu. Ni mwongozo kwa watawala unaosimulia jinsi wanapaswa kutenga na kutumia vipengele vya uzalishaji kwa faida ya biashara. Awali, iliweza kuwasaidia mameneja kuamua ni aina gani ya biashara wangetaka kuanzisha.
Jinsi ya kutekeleza sera na mikakati
[hariri | hariri chanzo]- Sera na mikakati yote lazima ijadiliwe na wasimamizi na wafanyakazi wote.
- Mameneja wanapaswa kuelewa wapi na jinsi gani wanaweza kutekeleza sera na mikakati yao.
- Mpango wa utekelezaji lazima uundwe kwa kila idara.
- Sera na mikakati lazima irekebishwe mara kwa mara.
- Mipango ya dharura lazima iundwe endapo mazingira yatabadilika.
- Tathmini ya maendeleo inapaswa kufanywa mara kwa mara na mameneja wa ngazi ya juu.
- Mazingira mema na roho ya umoja inahitajika katika biashara.
- Misheni, malengo, uwezo na udhaifu wa kila idara lazima ikadiriwe ili kuamua majukumu yao katika kufanikisha misheni ya biashara.
- Mbinu ya kutabiri huleta picha ya kuaminika mazingira ya usoni ya biashara.
- Kitengo cha mipango ni lazima kiundwe ili kuhakikisha kuwa mipango yote ni thabiti na kwamba sera na mikakati inalenga kufanikisha misheni na malengo sawa.
- Mipango ya dharura lazima iendelezwe, endapo itahitajika kutumika.
Sera zote lazima zijadiliwe na wasimamizi wote pamoja na wafanyakazi wote wanaohitajika katika utekelezaji wa sera.
- Mabadiliko ya shirika hufanikishwa kimkakati kwa utekelezaji wa mpango wa utekelezaji wa hatua nane uliobuniwa naye John P. Kotter: Kuongeza uharaka, kupata maono sahihi, kuwasilisha kununua, kuwezesha utekelezaji, unda ushindi wa muda mfupi, usife moyo, na kufanya mabadiliko yadumu.
Ambapo sera na mikakati huafiki katika mchakato wa mipango
[hariri | hariri chanzo]- Wao huwapa mameneja wa ngazi ya kati na chini wazo zuri juu ya mipango ya usoni ya kila idara.
- Mkakati unaundwa ambapo mipango na maamuzi hufanywa.
- Usimamizi wa ngazi ya chini na kati wanaweza kuongeza mipango yao wenyewe kwa mipango ya kimkakati ya biashara.
Ngazi za Usimamizi wa vitengo vingi
[hariri | hariri chanzo]Usimamizi wa shirika kubwa unaweza kuwa na ngazi zifuatazo:
- Usimamizi Mwandamizi (au "usimamizi wa juu" au "Usimamizi wa kichwani")
- Usimamizi wa Katikati
- Usimamizi wa ngazi ya chini, kama vile msimamiziau kiongozi wa timu
- Akida
- Wafanyakazi wa kawaida sana
- Usimamizi wa ngazi ya juu
- Unahitaji ujuzi wa kina wa majukumu ya usimamizi na ujuzi.
- Wanapaswa kuwa anajua sana masuala ya nje kama vile masoko.
- Asili ya maamuzi yao kwa ujumla ni ya muda mrefu.
- Maamuzi yao yanafanywa kwa kutumia michakato inayohusisha uchambuzi, agizo, dhana na / au kitabia / kushiriki
- Wao wanawajibikia maamuzi ya kimkakati.
- Wanapaswa kuuchunguza mpango na kuona kwamba mpango unaweza kuwa na ufanisi katika siku zijazo.
- Wao kiasili ni watendaji.
Wasimamizi wa ngazi ya juu ni kama vile wakurugenzi, rais wa kampuni,makamu wa rais wa kampuni, mkurugenzi mtendaji (CEO), na maafisa wakuu wa kampuni kama vile afisa mkuu wa fedha, afisa mkuu wa teknolojia n.k.
- Usimamizi wa katikati
- Mameneja wa kiwango cha kati wana ufahamu maalum wa kazi fulani za usimamizi.
- Wanawajibika kutekeleza maamuzi yaliyotolewa na uongozi wa ngazi ya juu.
Usimamizi wa ngazi ya kati unajumuisha meneja mkuu (kwa Kingereza General Manager), meneja wa tawi, na meneja wa idara. Meneja Washirikishi (kwa Kingereza Affiliate Managers) pia wako katika kitengo hiki kwa utaalum wa usimamizi shirirkishi.[8][9]
- Usimamizi wa ngazi ya chini
- Ngazi hii ya usimamizi uhakikisha kuwa maamuzi na mipango iliyochukuliwa na ngazi hizo zingine imetekelezwa.
- Maamuzi ya mameneja wa ngazi ya chini kwa ujumla huwa ya muda mfupi.
Wanaojumuishwa katika kitengo nikama vile viongozi wa vitengo tofauti tofauti
- Akida / mkono ongozi
- Ni kundi la watu walio na usimamizi wa moja kwa moja juu ya wafanyakazi katika afisi ya kiwandani, sehemu ya mauzo au kundi la kazi au maeneo ya shughuli.
Katika kitengo hiki kuna waangalizi (kwa kingereza Supervisors), wanyapara, na viongozi wa timu
- Wafanyakazi wa kawaida
- Wajibu wa watu walio kwenye kundi hili ni finyu zaidi na ni mahsusi zaidi hata kuliko wa maakida.
Maeneo na makundi ya utekelezaji wa usimamizi
[hariri | hariri chanzo]Tazama pia
[hariri | hariri chanzo]Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ Kwa Kiingereza to manage linatoka katika neno la Kiitalia maneggiare (kudhibiti - hasa farasi), lugha ambayo kwa upande wake hupata neno hili kutoka Kilatini manus (mkono). Neno la Kifaransa mesnagement (baadaye ménagement) lilichangia maendeleo katika maana ya neno la Kiingereza management katika karne ya 17 na 18. Tazama Kamusi ya Kiingereza ya Oxford
- ↑ Biashara ya kiufundi : Mafunzo, Kukuza na kuhamasisha Watu: 'Training, Developing and Motivating People' na Richard Barrett - Business & Economics - 2003. - ukurasa wa 51.
- ↑ Administration industrielle et générale - prévoyance shirika - commandement, uratibu - contrôle, Paris: Dunod, 1966
- ↑ 4.0 4.1 Gomez-Mejia, Luis R. (2008). Management: People, Performance, Change, 3rd edition. New York, New York USA: McGraw-Hill. ku. 19. ISBN 978-0-07-302743-2.
{{cite book}}
: Unknown parameter|coauthors=
ignored (|author=
suggested) (help) - ↑ 5.0 5.1 5.2 Gomez-Mejia, Luis R. (2008). Management: People, Performance, Change, 3rd edition. New York, New York USA: McGraw-Hill. ku. 20. ISBN 978-0-07-302743-2.
{{cite book}}
: Unknown parameter|coauthors=
ignored (|author=
suggested) (help) - ↑ Craig, S. (2009, 29 Januari). Kesi yake Merrill Bonus yazidi kupanuka huku mkataba ukilemewa Makala ya Wall Street. [1]
- ↑ Kotter, John P. & Dan S. Kohen. (2002). Moyo wa mabadiliko. Boston: Uchapishaji wa Shule ya Kibiashara ya Harvard
- ↑ "What is an Affiliate Manager? - Definition & Information". Marketing Terms (kwa American English). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2019-07-11. Iliwekwa mnamo 2019-01-20.
- ↑ Bradley Keys (2018-08-01). "What do Affiliate Managers Do All Day?". Advertise Purple (kwa American English). Iliwekwa mnamo 2019-01-20.
Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]- Masomo ya Usimamizi Ilihifadhiwa 31 Januari 2008 kwenye Wayback Machine. katika MIT Sloan, OpenCourseWare
- Utafiti wa Mashirika: Bibliography Database and Maps Ilihifadhiwa 18 Februari 2019 kwenye Wayback Machine.
- ATMAE Ilihifadhiwa 11 Julai 2011 kwenye Wayback Machine. The Association for Technology, Management, and Applied Engineering