Nenda kwa yaliyomo

Stefano wa Hungaria

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mt. Stefano wa Hungaria.

Stefano I wa Hungaria (kwa Kihungaria István; kwa Kilatini Stephanus; Esztergom, Hungaria, 967 au 969 au 975 – Esztergom [1][2][3] au Székesfehérvár, 15 Agosti 1038) kabla hajabatizwa aliitwa Vajk na kuwa Mtawala mkuu wa Wahungaria (9971000).

Papa Silvesta II alimfanya mfalme wa kwanza wa Hungaria (1000–1038). Hapo alieneza sana ufalme wake pamoja na Kanisa Katoliki, akilipanga upya na kulipatia mali na monasteri ili kufanya wananchi wake, aliowatawala kwa haki na amani, wajiunge nalo [4].

Papa Gregori VII alimtangaza mtakatifu pamoja na mwanae, Emeriko wa Hungaria na Jeradi Sagredo, mwinjilishaji wa nchi hiyo, tarehe 20 Agosti 1083.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 16 Agosti[5].

Tazama pia

[hariri | hariri chanzo]
  1. "István halála". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2009-02-12. Iliwekwa mnamo 2012-09-08.
  2. Esztergom.hu
  3. Hankó Ildikó: Királyaink Tömegsírban
  4. https://www.santiebeati.it/dettaglio/28850
  5. Martyrologium Romanum

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]
WikiMedia Commons
WikiMedia Commons
Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.