Nenda kwa yaliyomo

Sara

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Abrahamu akimshauri Sara (18961902 hivi kadiri ya James Tissot).
Sara (kulia) akisikiliza maongezi ya Abrahamu na wageni wake (malaika watatu waliomuahidia mtoto wa kiume).
Kaburi la Sara, 1911.

Sara (kwa Kiebrania שָׂרָה, Śārā, awali Sarai) katika Biblia anajulikana kama mke tasa wa Abrahamu ambaye kwa imani katika ukongwe wake alijaliwa kumzaa Isaka, baba wa Israeli, taifa teule la Mungu. Habari hizo zinapatikana hasa katika kitabu cha Mwanzo.

Jina lake linamaanisha mwanamke wa ukoo bora.

Tangu kale anaheshimiwa na Waorthodoksi wa Mashariki kama mtakatifu.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 19 Agosti.

Katika Agano Jipya

[hariri | hariri chanzo]

Waraka wa kwanza wa Petro unamsifu Sara kwa kumtii mumewe[1]

Waraka kwa Waebrania unamsifu kwa imani yake.[2]

Mtume Paulo anamtaja katika nyaraka zake kwa Wagalatia[3] na kwa Warumi[4] katika kueleza tofauti kati ya Agano la Kale na Agano Jipya.

Tazama pia

[hariri | hariri chanzo]
  1. 1 Pet 3:6
  2. Eb 11:11
  3. Gal 4:22-23
  4. Rom 4:19 na 9:9
Makala hii kuhusu mtu wa Biblia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Sara kama habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.