Nenda kwa yaliyomo

Mataifa ya Kiturki

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Makala hii kuhusu "Mataifa ya Kiturki" inatumia neno au maneno ambayo si ya kawaida; matumizi yake ni jaribio kwa jambo linalotajwa.
Wasomaji wanaombwa kuchangia mawazo yao.

Kamusi za Kiswahili ama zinatofautiana kuhusu matumizi ya neno hili au hazieleweki au hazina neno kwa jambo linalojadiliwa.

Nchi huru ambako mataifa ya Kiturki huwa na wakazi wengi

Mataifa ya Kiturki ni kundi la mataifa na makabila yanayotumia mojawapo ya lugha za Kiturki. Katika makala hii tunawaita "Waturki"[1]. Taifa kubwa katika kundi hilo ni Waturuki, raia wa nchi ya Uturuki.

Nchi nyingine ambako watu wengi ni kutoka mataifa ya Kiturki ni pamoja na Kazakhstan, Uzbekistan, Azerbaijan na Turkmenistan. [2]

Lakini wako pia katika Siberia (Urusi), katika milima ya Kaukazi, Iraki, Iran, Afghanistan, Kirgizia na China ya magharibi.

Wengi wao wanaweza kuwasiliana hata kama wanatoka nchi tofauti, kwa sababu lugha zao ni za karibu na kuna maneno mengi ya pamoja.

  1. Neno "Turki" ni jaribio na hadi sasa hakuna namna katika Kiswahili sanifu kutofautisha kati ya watu wa nchi ya Uturuki (tunawaita hapa Waturuki; Kiingereza Turks, people of Turkey) na watu wanaotumia mojawapo ya lugha tunazoita "za Kiturki" (Turkic languages, Turkic peoples). Kwa hiyo tunajaribu kutofautisha kati ya "Waturuki" wa Uturuki, na "Waturki" wanaotumia mojawapo ya lugha ambazo ni karibu kati yake.
  2. https://dergipark.org.tr/tr/download/article-file/785506