Kit Mikayi
Kit-Mikayi (pia hutajwa kama Kit Mikayi, Kitmikayi na Kitmikaye) ni mwamba mkubwa uliyoko kwenye barabara ya Kisumu-Bondo magharibi mwa Kenya, karibu kilometa 29 magharibi mwa Kisumu. Kit-mikayi inamaanisha "Mawe ya mke wa kwanza" katika Dholuo, lugha ya Waluo.
Historia
[hariri | hariri chanzo]Hadithi inayoelezea kuhusu Kit Mikayi ni kwamba: Wakati mrefu uliopita, kulikuwa na mzee aliyeitwa Ngeso aliyekuwa amelipenda sana jiwe hilo. Kila siku, angeamka asubuhi, aende pale penye jiwe na ashinde hapo siku nzima na hili lingemlazimisha mkewe ampelekee kiamsha-kinya na chakula cha mchana kila siku. Mzee huyu alilipenda sana jiwe hili kiasi kwamba watu walipomuuliza mkewe alipokuwa, mkewe aliwajibu kuwa alikuwa ameenda kwa mkewe wa kwanza (Mikayi). Hili lilisababisha jiwe liitwe Kit Mikayi (Jiwe la Mke wa kwanza).
Maelezeo zaidi yanaelezea kuwa kulingana na muundo wake, jiwe hili liliwakilisha familia ya kitamaduni ya kiluo ya mabibi wengi, iliyokuwa na nyumba ya bibi wa kwanza (Mikayi) ilijengwa katikati mwa boma, nyumba ya bibi wa pili (Nyachira) ilijengwa katika upande wa kulia na nyumba ya bibi wa tatu (Reru) ilijenga katika upande wa kushoto. Jiwe hili linaweza pia kuwakilisha familia ndogo ambapo, Baba (Ngeso) ndiye jiwe la kati akifuatwa Bibi wa kwanza (Mikayi), Bibi wa pili (Nyachira) halafu Bibi wa tatu (Reru) na mbele kabisa, walikuwa na mtoto aliyewakilisha Simba (nyumba ya kifungua-mimba wa kiume wa boma)
Maelezeo na mahali
[hariri | hariri chanzo]Kit-Mikayi ni muundo wa mawe - jiwe la mita 70 - karibu na barabara ya Kisumu-Bondo takriban kilometa 29 magharibi mwa Kisumu (kuelekea soko la Kombewa na kabla ya kufikia daraja la mto Nyamgun) katika kitongoji cha Kakelo.
Umuhimu
[hariri | hariri chanzo]Wenyeji wanaoishi karibu na mwamba huo wanajulikana kama jamii ya Wajaluo-Kakello. Eneo hili limehusishwa na dhabihu na hadithi nyingi kutoka nyakati za kabla ya ukristo, hasa hadithi kueleza maana ya jina lake.
Kit-Mikayi ni kituo kikuu cha kuonea, hasa kati ya makabila ya jirani ya Waluo. Pia imekuwa pahali pa kuombea kwa wafuasi wa injili ya Legio Maria ambao huja kuomba na kufunga kwa wiki kadhaa.
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]Makala hii kuhusu maeneo ya Kenya bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Kit Mikayi kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |