Imamu
Imamu (kutoka Kiarabu: إمام imām) ni istilahi ya Kiarabu yenye maana mbalimbali. Mara nyingi inamtaja kiongozi wa Kiislam, kama kiongozi wa msikiti au wa jamii. Maana ya msingi ni yule anayetoa mwongozo akistahili kufuatwa; kwa maana isiyo ya kidini neno hili linaweza kutaja pia timazi au kamba inayotumiwa kuelekeza mwendo wa matofali wakati wa kujenga nyumba au ukuta.[1]
Imamu anaitwa yule anayeongoza sala wakati wa swala ya Kiislamu.
Wasunni
[hariri | hariri chanzo]Kati ya Wasunni istilahi hilo linatumiwa kumtaja mtaalamu wa kidini, mara nyingi kama cheo cha heshima kwa waanzilishi wa madhab nne za Wasunni yaani Hanafi, Maliki, Shafi'i na Hanbali.[2]
Washia
[hariri | hariri chanzo]Kati ya Waislamu Washia "imamu" ni hasa yule kiongozi mmoja wa waumini anayetoka katika familia ya Mtume Mohammed. Kwa Washia Waismaili imamu ndiye Aga Khan. Kwa Washia Waithnashara maimamu ni hasa wafuasi 12 wa Muhammad kuanzia Ali ibn Abu Talib na watoto pamoja na wajukuu wake hadi Muhammad ibn al-Hassan anayeaminiwa kuwa imamu wa sasa aliyeingia katika hali ya kujificha wakisubiri kurudi kwake atakapoonekana tena[3] .
Huko Iran pia Ruhollah Khomeini anaitwa "imamu" (kwa matamshi yao "emam")
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ [https://archive.org/details/LANESARABICENGLISHLEXICONDIGITIZEDTEXTVERSION Lane, Edward William: Arabic – English Lexicon], Perseus Collection Arabic Materials, Attribution-ShareAlike 3.0 United States - CREATIVE COMMONS, Online Version, Released Digitized Text Version v1.1, Kitabu cha kwanza uk. 90-92
- ↑ Rabb, Intisar A. (2009). "Fiqh". In John L. Esposito. The Oxford Encyclopedia of the Islamic World. Oxford: Oxford University Press. . .
- ↑ Virani, Shafique. "Khayrkhvāh-i Harātī". Encyclopaedia of Islam (kwa Kiingereza).
Tovuti za nje
[hariri | hariri chanzo]- Detailed description of the Shiite belief
- Graphical illustration of the Shia sects Archived 2004-10-25 at the Wayback Machine
- List of Sunni Imams
- [http://web.archive.org/20211226195343/http://www.the-imam.com/ Ilihifadhiwa 26 Desemba 2021 kwenye Wayback Machine. The Imam Movie]