Nenda kwa yaliyomo

Ian Duncan

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Ian Duncan
World Rally Championship record
Active years1983–1999
TeamsSubaru, Toyota
Rallies15
Championships0
Rally wins1
Podiums4
Stage wins4
Total points80
First rally1983 Safari Rally
First win1994 Safari Rally
Last rally1999 Safari Rally

Ian Duncan (alizaliwa 23 Juni 1961) ni mmoja ya madereva wa rally ambao wamefanikiwa sana nchini Kenya. Alikuwa bingwa wa Rally nchini Kenya mara tano (1987, 1988, 1989, 1991 na 2000), na alifanikiwa kupata ushindi wa "outright" katika michuano wa magari ya Rally wa Dunia aliposhinda shindano la 42 la Trustbank Safari Rally mwaka wa 1994. Hii ilikuwa moja kati ya tamati zake za nafasi kumi za kwanza mfululizo katika tukio hilo kuanzia mwaka wa 1990 hadi mwaka wa 1996, licha ya kiwango chake cha sifa mbaya.

Ian alilelewa katika shamba la wazazi wake katika sehemu ya Limuru. Ladha yake ya kwanza ya kuendesha gari ilitokea wakati alikuwa na umri wa miaka karibu kumi, huku akimsaidia mama yake wakati alikwama katika barabara za shamba wakati wa mvua. Alihudhuria Shule ya Upili ya St Mary's, kwani nia yake zaidi ilikuwa katika kutengeneza magari na pikipiki. Pia alishiriki katika Motocross na kushinda taji la 125cc la kitaifa miaka ya 1979 na 1980. Alishiriki katika Safari Rally kwa mara ya kwanza mwaka wa 1983 huku akiliendeaha gari la Nissan Pick-Up huku naibu dereva wake akiwa Gavin Bennett, na alimaliza katika nafasi ya tisa na huku akipata ushindi wa darasa na kupata usikivu wa watu rally.[1]

Ushindi wake wa kwanza wa kitaifa wa Rally ulikuwa katika mji wa Nakuru mwaka wa 1987 wakati alikuwa anaendesha gari ya aina ya Toyota Celica Cam Twin Turbo huku naibu dereva wake akiwa Ian Munro. Duncan alishinda mchuano wake wa kwanza wa kitaifa mwaka huo huo kwani alishinda mashindano mengi. Alishinda tuzo la mwendesha motokaa wa mwaka wa kitaifa mwaka wa 1987.

Alishiriki kwa kutumia Group A Subaru Legacy na Toyota Celica Turbo 4WD katika miaka ya 1990. Mbali na Safari Rally, alishiriki katika mikutano ya kampeni za WRC mara chache tu. Tokeo lake bora lilikuwa kumaliza katika nafasi ya 8 kwa jumla na kushinda darasala kundi N katika shindano la safari rally la Acropolis Rally mwaka wa 1990 nchini Ugiriki huku naibu dereva wake akiwa Yvonne Mehta (mke wa Shekhar Mehta).

Baadaye alianza kuendesha gari la aina ya Toyota Hilux ambalo lilikuwa na injini ya lita 4.5 na alilitumia katika mchuano wa rally wa kitaifa wa Kenya (Kenya National Rally Championship (KNRC)). Mnamo Novemba mwaka wa 2006 Duncan alishinda Guru Nanak Rally na kuwa dereva wa kwanza kushinda taji la KNRC kwa mara ya kumi. Alipewa adhabu ya asilimia nne ya muda kwa sababu hakuwa ameliandikisha gari lake. Aliendeleza rekodi yake mwaka wa 2007 na kwa mara nyingine tena akashinda Guru Nanak Rally.

Duncan ameshinda tukio la Rhino Charge off-road katika miaka ya 1998, 2006 na 2007. Ameshiriki katika mashindano ya pikipiki. Mnamo mwaka wa 2003, alichukua nafasi ya pili katika Kenya Enduro, Motocross na vilevile Michuano ya rally .[2]

Alitumia gari lake mpya, Nissan Patrol Pick-up, mnamo Oktoba mwaka wa 2008. Mwaka wa 2008 pia alishinda mchuano wa kitaifa wa autocross. Mnamo mwaka wa 2009, miaka 15 baada ya kushinda Safari Rally halisi, Duncan alishinda Safari classic rally huku akiliendesha gari la mwaka wa 1967 la Ford Mustang huku naibu dereva wake akiwa naibu dereva wake wa sasa, Amaar Slatch. Bingwa mtetezi Bjørn Waldegård alimaliza katika nafasi ya pili.

Ushindi wa WRC

[hariri | hariri chanzo]
 #  Tukio Msimu Naibu-dereva Gari
1 Kenya 42 Trustbank Safari Rally 1994 David Williamson Toyota Celica Turbo 4WD
  1. Daily Nation, 26 Desemba 2009: Duncan's mustang ride to victory
  2. Daily Nation, 29 Desemba 2003: Rose takes over KNRC

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]
Makala hii kuhusu mambo ya michezo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu zaidi kuhusu Ian Duncan kama historia yake, uenezi au kanuni zake?
Labda unaona katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine habari zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.