Nenda kwa yaliyomo

Gobani

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Gobani (alifariki Ufaransa, 670) alikuwa mmonaki padri wa Ukristo wa Kiselti kutoka Ireland.

Kama alivyothibitisha Beda Mheshimiwa[1], alikuwa mwanafunzi wa Fursei abati, aliyefanya kazi kubwa kueneza imani na umonaki kotekote katika visiwa vya Britania, hasa kati ya Waanglia[2][3].

Huyo alipohamia Ufaransa, Gobani alimfuata; hatimaye akawa mkaapweke kwenye msitu wa Voas, karibu na kijiji chenye jina lake, Saint-Gobain, Aisne.

Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu, pengine mfiadini.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 20 Juni[4].

Tazama pia

[hariri | hariri chanzo]
  1. https://www.santiebeati.it/dettaglio/58620
  2. "St Fursey". Cathedral.org.uk. 2015-02-25. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2015-02-04. Iliwekwa mnamo 2015-03-01.
  3. "St. Fursey". Libraryireland.com. Iliwekwa mnamo 2015-03-01.
  4. Martyrologium Romanum
Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.