Nenda kwa yaliyomo

Leonardo da Vinci

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

'

Leonardo da Vinci
Leonardo da Vinci alivyojichora
Amezaliwa15 Aprili 1452
Amefariki2 Mei 1519
Kazi yakemwanahisabati, mhandisi, mwanasayansi, mgunduzi, mwanaanatomi, mchoraji, mchongaji, msanifuujenzi, mwanabotania, mwanamuziki na mwandishi


Leonardo Da Vinci (Vinci, Toscana, Italia, 15 Aprili 1452Amboise, Ufaransa, 2 Mei 1519) alikuwa mtu mwenye vipaji vingi[1] kutoka nchini Italia.

Kifupi, alikuwa mwanahisabati, mhandisi, mwanasayansi, mgunduzi, mwanaanatomi, mchoraji, mchongaji, msanifuujenzi, mwanabotania, mwanamuziki na mwandishi.

Ndiye mwakilishi bora wa tapo la Renaissance.

Leonardo alikuwa mdadisi wa kila kitu asilia. Alitaka kujua kila kitu kinavyofanya kazi. Alikuwa hodari sana katika kusoma, kuunda na kutengeneza vitu vya aina mbalimbali tena vya kupendeza.[2]

Mwanahistoria wa sanaa Helen Gardner alisema hakuna mtu aliyewahi kuwa kama yeye kwa sababu alikuwa na shauku na vitu vingi sana: "...Akili yake na utu wake vinaonekana kuwa zaidi ya mtu, ni mtu wa ajabu na tofauti".

Leonardo siku zote alikuwa akifiria kugundua mambo mapya. Vitu vingi alivyogundua havikuwahi kufanywa. Hata hivyo, tunajua fikra zake, kwa sababu aliweka kwenye vijitabu na kuandika na kuvichora mara kwa mara.

Baadhi ya nadharia alizofikiria ni pamoja na helikopta, kifaru, baiskeli, kikokotoo, roboti na vifaa vinavyogeuza nishati ya jua kuwa umeme.

Leonardo aliweza kufanya vitu vya aina nyingi vya kijanja, lakini alikuwa maarufu sana kama mchoraji. Watu wengi hufikiria kwamba Leonardo alikuwa mmoja kati ya wachoraji bora wa historia yote. Amefanya michoro mingi sana. Miongoni mwa picha zake, mbili zilizo maarufu zaidi duniani ni Mona Lisa na Karamu ya mwisho.

Mchoro mwingine unaojulikana sana ni Vitruvian Man. Unajulikana sana hata Homer Simpson na Garfield ambazo zilichorwa kwa mraba na mzunguko ili kuonekana kama mchoro.

Utoto, 1452–1466

[hariri | hariri chanzo]
Mchoro uliojulikana awali wa Leonardo, Arno Valley, (1473) - Uffizi, Florence, Italia.

Leonardo alizaliwa tarehe 15 Aprili 1452, mkoani Toscana, katika mji mdogo wa kilimani wa Vinci, katika mabonde ya Mto Arno, karibu na Florence nchini Italia.

Babu yake, Ser Antonio, anajivunia kwa kuweka kumbukumbu ya maelezo. Wazazi wa Leonardo walikuwa hawajaoana. Baba yake alikuwa mwanasheria, Messer Piero Fruosino di Antonio da Vinci.[3][4] Mama yake, Caterina, alikuwa mhudumu. Yawezekana alikuwa mtumwa kutoka Mashariki ya Kati.[5][6] Jina kamili la Leonardo lilikuwa "Leonardo di ser Piero da Vinci", ambalo lina manaa ya "Leonardo, mtoto wa Bwana Piero kutoka Vinci".

Leonardo alitumia miaka yake mitano ya awali akiishi katika nyumba ya shambani na mama yake. Halafu akaja kuishi Vinci na baba yake, mke wa baba yake aliyeitwa Albiera, mabibi/mababu zake na wajomba zake, Francesco.

Wakati Leonardo ameshakua, aliandika vitu viwili tu kuhusu maisha yake ya utotoni. Alikumbuka kwamba alivyokuwa amelala kwenye kitanda chake cha watoto nje ya nyumba yao ndege mkubwa alikuwa akipaa na kumzungukazunguka juu yake. Mikia yake ikawa inamfutafuta sura yake.[7] Kumbukumbu nyingine muhimu ya Leonardo ilikuwa vipi aligundua pango milimani wakati anapeleleza. Alikuwa na hofu kubwa sana huenda kukawa na kiumbe kikubwa cha ajabu kimejificha mle ndani ya pango. Lakini pia alikuwa na hamu na shauku ya kujua kilichopo mle ndani.

Giorgio Vasari aliandika kuhusu maisha ya Leonardo kwa ufupi baada ya kifo chake. Ameelezea hadithi za kuvutia kibao kuhusu utundu aliokuwa nao Leonardo. Anasema kwamba Leonardo alichora bamba la taarifa la mbao-mzunguko likiwa na picha ya mijoka inayotema moto. Messer Piero alichukua michoro ya mwanawe hadi Florence na kuiuza kwa wauzaji wa bidhaa za kisanaa.[8]

Ujana na utu uzima

[hariri | hariri chanzo]
Ubatizo wa Kristo kadiri ya Verrocchio na Leonardo (1472–1475) — Uffizi.

Leonardo alianza kuchora tangu yungali bado kijana. Alifunzwa usanii na mchongaji na mchoraji Verrocchio.

Sehemu kubwa ya maisha yake alimtumikia tajiri mmoja maarufu wa Italia.

Mwaka 1516 Leonardo alikwenda Amboise, Ufaransa, baada ya kupata mwaliko kutoka kwa mfalme Fransisko I. Kati ya mizigo aliyosafiri nayo ulikuwemo mchoro maarufu wa Monalisa.

Leonardo aliishi mjini Amboise, katika nyumba yake nzuri aliyopewa na Mfalme huyo wa Ufaransa, miaka yake ya mwisho, toka mwaka huo mpaka mwaka 1519.

Afya yake haikuwa nzuri kwa sababu alipatwa na ugonjwa wa kiharusi toka mwaka 1517, lakini taarifa za ugonjwa wake zikatolewa wiki chache kabla ya kifo chake.

Alifariki huko Amboise tarehe 2 Mei 1519 akiwa na umri wa miaka 67, akazikwa St. Hubert.

  1. Vasari, Boltraffio, Castiglione, "Anonimo" Gaddiano, Berensen, Taine, Fuseli, Rio, Bortolon, etc as quoted in della Chiesa, see Bibliography
  2. Gardner, Helen (1970), Art through the Ages, Harcourt, Brace and World
  3. Vezzosi, Alessandro, Leonardo da Vinci: Renaissance Man
  4. Angela Ottino della Chiesa, The Complete Paintings of Leonardo da Vinci
  5. According to Alessandro Vezzosi, Head of the Leonardo Museum in Vinci, Piero may have owned a Middle Eastern slave called Caterina. A study of Leonardo's fingerprint suggests that he may have had Middle Eatern blood.Experts Reconstruct Leonardo Fingerprint" 12 Desemba 2001
  6. Experts Reconstruct Leonardo Fingerprint, The Associated Press, iliwekwa mnamo 2007-12-14
  7. Bortolon, Liana (1967), The Life and Times of Leonardo, London: Paul Hamlyn
  8. Giorgio Vasari, Lives of the Artists, 1568; this edition Penguin Classics, trans. George Bull 1965, ISBN 0-14-044164-6

Viungo vya Nje

[hariri | hariri chanzo]
Makala hii kuhusu mwanasayansi fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Leonardo da Vinci kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.