Jimbo Katoliki la Kondoa
Mandhari
Jimbo Katoliki la Kondoa (kwa Kilatini "Dioecesis Kondoaënsis") ni mojawapo kati ya majimbo 34 ya Kanisa Katoliki nchini Tanzania, katika mkoa wa Dodoma, hususan wilaya ya Kondoa.
Kama majimbo hayo yote, linafuata mapokeo ya Kilatini ya Kanisa la Roma.
Historia
[hariri | hariri chanzo]Jimbo hilo liliundwa rasmi tarehe 12 Machi 2011 kutokana na Jimbo Katoliki la Dodoma kupewa kama askofu wake wa kwanza Bernardine Mfumbusa.
Linahusiana na jimbo kuu la Dodoma.
Takwimu
[hariri | hariri chanzo]Waamini wake ni 46.067 kati ya wakazi 541.345 (sawa na 8.5%) wa eneo lake la kilometa mraba 13,210, ambao wengi wao ni Waislamu.
Jimbo lina mapadri 17, ambao kati yao 15 ni wanajimbo na 2 tu ni watawa. Hivyo kwa wastani kila padri anahudumia Wakatoliki 2.710 katika parokia 9.
Jimbo lina masista 87.
Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]- Catholic Hierarchy katika ukurasa [1]
- Hati ya Papa Benedikto XVI Cum ad provehendam
Makala hii kuhusu Kanisa Katoliki bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Jimbo Katoliki la Kondoa kama historia yake au maelezo zaidi? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |