Nenda kwa yaliyomo

Tengamaji

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Pitio kulingana na tarehe 10:55, 16 Juni 2016 na Kipala (majadiliano | michango) (Marejeo)
(tofauti) ← Pitio lililotangulia | Toleo la sasa (tofauti) | Pitio linalofuata → (tofauti)
Beseni ya mto Lotro, Romania; mstari mwekundu ni tengamaji
Ramani ya beseni kubwa kwenye bara la Afrika (tahajia ya Kijerumani)

Tengamaji (ing. drainage divide[1]) ni sehemu za juu zinazotenganisha beseni za mito inayokusanya maji ya eneo fulani. Kila upande wa tengamaji maji yote hutirikika kuelekea mto mkubwa unaobeba maji hadi baharini, au kwenda ziwa fulani mfano Ziwa Chad, Bahari ya Kaspi lisilo na uhusiano na bahari.

Kwa lugha nyingine tengamaji ni sehemu ambako matone mawili ya mvua yanayoanguka mahali pa karibu yatatiririka mtelemko kuelekea mito tofauti.

Tengamaji mara nyingi ni safu ya milima au vilima kwa mfano ni safu za Uporoto na Kipengere katika Tanzania Kusini zinatotenganisha maji kati ya beseni za Ruaha Mkuu na Mto Zambezi (kupitia Ziwa Nyasa). Tengamaji katika tambarare haitambuliki kirahisi hivi.

Katika elimu ya hidrolojia wataalamu hutofautisha ngazi mbalimbali

  • tengamaji kuu au tengamaji ya kibara: mstari unaopita katika bara na kusababisha mvua kuelekea bahari tofauti; kwa mfano tengamaji kuu ya Amerika Kaskazini inafuata safu ya Rocky Mountains na kugawa bara lote kati ya beseni kuu za Atlantiki na Pasifiki. Ndani ya beseni hizi kuu kuna tena beseni za mito tofauti inayofikisha maji baharini.

Barani Afrika tengamaji ya kibara muhimu ni tengamaji ya Kongo na Naili.

  • tengamaji kubwa ni mstari kati ya beseni za mito zinazokusanya maji ya eneo ka kuyafikisha katika bahari ileile; kwa mfano nchini Tanzania tengamaji kati ya Ruaha Kuu na Zambezi kwa sababu mito yote miwili inaishia katika Bahari Hindi. Nchini kenya mfano ni milima ya Aberdare ambayo ni tengamaji kati ya beseni za mto Athi na mto Tana inayoishia yote katika Bahari Hindi.
  • tengamaji ya kawaida ni mstari kati ya beseni mbili zitakazoungana baadaye, mfano tengamaji kati ya beseni ya Missouri na Missisippi ya juu. Mfano nchini Tanzania ni tengamaji kati ya beseni za Ruaha Mkuu na Mto Kilombero inayokutana baadaye kwenye Rufiji.


  1. Kwa lugha ya Kiingereza kuna majina yanayotofautiana katika Kiingereza cha Britania na Marekani, kama vile: water divide, divide, ridgeline, watershed, water parting