Nenda kwa yaliyomo

Zambezi (mto)

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Mto Zambezi)
Mto wa Zambezi
Mto Zambezi kwenye maporomoko ya Victoria
Mto Zambezi kwenye maporomoko ya Victoria
Chanzo karibu na Mwinilunga, Zambia
Mdomo Bahari ya Hindi
Nchi za beseni ya mto Zambia, Kongo, Angola, Namibia, Botswana, Zimbabwe, Msumbiji
Urefu km 2,574
Kimo cha chanzo m 1,500
Kiasi cha maji kinachotolewa mdomoni m³/s 7,000
Eneo la beseni (km²) km² 1,570,000

Zambezi ni kati ya mito mirefu ya Afrika ikishika nafasi ya nne baada ya Nile, Kongo na Niger. Ni mto mrefu wa Afrika wa kuingia Bahari Hindi.

Beseni lake lina km² 1,570,000 au nusu ya mto Nile. Chanzo chake kiko Zambia, halafu mto unapita Angola mpakani na Namibia, Botswana, Zambia na Zimbabwe kwenda Msumbiji inapofikia Bahari Hindi katika delta ya km² 880.

Kwenye mwendo wa Zambezi pana maporomoko kadhaa hasa maporomoko ya Victoria Falls. Mengine ni maporomoko ya Chavuma mpakani mwa Zambia na Angola, halafu Ngonye Falls karibu na Sioma, Zambia ya magharibi.

Zambezi ina madaraja matano pekee kati ya chanzo na mdomo mahali pafuatapo: Chinyingi, Katima Mulilo, Victoria Falls, Chirundu na Tete.

Zambezi ni chanzo cha umeme kwa ajili ya sehemu kubwa ya Afrika ya Kusini. Umeme unatengenezwa kwa nishati ya maji huko lambo la Kariba (Zambia) na lambo la Cabora-Bassa (Msumbiji).

Matawimto

[hariri | hariri chanzo]

Matawimto muhimu zaidi ni Cuando, Kafue, Luangwa na Shire.

Miji muhimu mtoni

[hariri | hariri chanzo]

Tazama pia

[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]
Makala hii kuhusu maeneo ya Afrika bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Zambezi (mto) kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.