Euro
Euro ni sarafu ya pamoja katika baadhi ya nchi za Ulaya. Wakazi wake 350,000,000 (2023) wanatumia kwa kawaida pesa hiyo. Watu wengine 210,000,000 wanatumia pesa zilizoungwa na euro, hasa barani Afrika.
Tangu mwaka 2002 nchi 13 za EU zilifuta sarafu ya kitaifa ili kutumia Euro tu. Siku hizi ni 20.
Euro moja imegawanyika katika senti 100.
Kuna benknoti za € 5 (kijivu), € 10 (nyekundu), € 20 (buluu), € 50 (machungwa), € 100 (kijani), € 200 (njano), € 500 (nyekundu).
Kuna sarafu za metali 8 za € 0,01, € 0,02, € 0,05, € 0,10, € 0,20, € 0,50, € 1, € 2.
Pesa ya karatasi inatolewa na benki kuu ya Ulaya na ni sawa kote.
Sarafu zinatolewa na nchi wanachama na zinatofautiana upande mmoja, lakini sarafu zote hutumika kote.
Ishara ya Euro
haririIshara ya Euro ni herufi ya Kigiriki epsilon (E) yenye mistari miwili ya kulala: €.
Nchi wanachama wa Euro
hariri- Austria
- Ubelgiji
- Ufini
- Ufaransa
- Ujerumani
- Ugiriki
- Ueire
- Italia
- Latvia
- Luxemburg
- Ureno
- Hispania
- Uholanzi
- Slovakia
- Slovenia
- Kupro
- Malta
- Estonia
- Lithuania
- Kroatia
Nchi 6 zifuatazo hutumia pia Euro kama pesa pekee bila kuwa sehemu za mapatano, ila 4 za kwanza kwa makubaliano maalumu, nyingine 2 kwa kujiamulia:
Pesa za nchi zifuatazo zimeungwa na Euro:
- Afrika: nchi 14 za CFA franc
- Kabo Verde - escudo
- Komori - franc
- Moroko - dirham
- Bosnia-Herzegovina - convertible mark
- Bulgaria - lev
- Denmark - krone
- Masedonia Kaskazini - denar
- Pasifiki: maeneo 3 ya CPF franc
-
Noti zote za Euro.
-
Sarafu zote kutoka Euro
-
Noti za Euro 5, 10, 20,50.
-
Noti na sarafu za Euro.
Viungo vya nje
hariri- Eurozone official portal
- The euro – Europa
- European Central Bank – Euro Exchange Rates
- European Central Bank
- Euro (Benknoti na historia) (Kiingereza) (Kijerumani)
Makala hii kuhusu mambo ya uchumi bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Euro kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |