Tuma ujumbe kwa faragha
Faragha yako ni muhimu sana kwetu. Ufumbaji wa mwanzo hadi mwisho huhakikisha ujumbe wako binafsi haufikiwi na mtu mwingine kando na unayemtumia.
Faragha yako ni muhimu sana kwetu. Ufumbaji wa mwanzo hadi mwisho huhakikisha ujumbe wako binafsi haufikiwi na mtu mwingine kando na unayemtumia.
Ujumbe na simu husalia kati yenu. Hakuna mtu mwingine anayeweza kuzisoma au kuzisikiliza, hata WhatsApp haiwezi.
Kando na ufumbaji wa mwisho-kwa-mwisho, tunaongeza hatua za ziada za ulinzi kwenye mazungumzo yako yote.
Unaweza kuchagua unachoshiriki, jinsi unavyoonekana mtandaoni, au anayeweza kuzungumza nawe.
Nenosiri hulinda soga zako nyingi za kibinafsi, ili mtu yeyote anayetumia simu yako asiweze kuziona.
Kipengele cha ujumbe unaotoweka kinakuwezesha kudhibiti ni ujumbe gani unaosalia na kwa muda gani, kwa kuchagua zitoweke baada ya kutuma.
Chuja barua taka na waasiliani wasiojulikana wasikupigie simu, ili uweze kuzingatia mazungumzo ambayo ni muhimu sana kwako.
Weka kwa faragha nakala zako zilizohifadhiwa mtandaoni. Washa ufumbaji wa nakala ili kuongeza usalama wa soga zako zinazohifadhiwa kwenye iCloud au Google Drive kwa kutumia ufumbaji wa mwisho hadi mwisho.
Teua kuonekana na watu unaowataka pekee. Unaweza kubadilisha mipangilio yako ya faragha ili kuchagua wanaoweza kuona ukiwa mtandaoni, na mara ya mwisho ulipotumia WhatsApp.
Linda akaunti yako dhidi ya wadukuzi na walaghai
na kukomesha soga zisizohitajika.