LSF

LSF

Non-profit Organizations

Dar es Salaam, Dar es Salaam 1,435 followers

Everyday Justice For Everyday Problems.

About us

Everyday Justice for Everyday Problems LSF is a non-profit organization established in 2011 to increase access to justice for all, in particular for women through a legal empowerment approach. The LSF channels its funding on an equal opportunity basis to organizations which provide legal aid and paralegal services on Tanzania mainland and Zanzibar. Our Commitment Promoting protection of human rights for all, with an emphasis on poor women, girls and other vulnerable groups. We enhance the availability, affordability, accessibility, and acceptability of quality legal aid services through paralegals and other legal aid providers. LSF works closely with the government of Tanzania at all levels, development partners, organizations involved in the provision of legal aid, including paralegal services and other like-minded stakeholders.

Industry
Non-profit Organizations
Company size
11-50 employees
Headquarters
Dar es Salaam, Dar es Salaam
Type
Nonprofit
Founded
2011

Locations

  • Primary

    Plot No. 1129 Chole Road, Masaki

    Dar es Salaam, Dar es Salaam, TZ

    Get directions

Employees at LSF

Updates

  • View organization page for LSF, graphic

    1,435 followers

    Wanawake wengi wanakabiliwa na changamoto za kuripoti ukatili wa kijinsia kutokana na hofu, unyanyapaa, ukosefu wa uelewa wa haki zao, na upatikanaji mdogo wa huduma za kisheria. Takwimu zinaonyesha kuwa chini ya asilimia 40 ya wanawake ndio wanaripoti unyanyasaji wanaokutana nao, huku wachache sana wakipata msaada wa kisheria. Ni muhimu kuelimisha jamii na kuweka mifumo rafiki ya kusaidia manusura wa ukatili wa kijinsia ili kuhakikisha haki inatendeka na kuimarisha usawa wa kijinsia. #FunguaPazia #TokomezaUkatili

    • No alternative text description for this image
  • View organization page for LSF, graphic

    1,435 followers

    Katika vijiji vingi vya Tanzania, wajane hukumbana na changamoto za kijamii na kiuchumi baada ya kufiwa na waume zao. Familia za mume mara nyingi huwafukuza kwenye ardhi au nyumba walizokuwa wakiishi, hali inayowanyima haki yao ya msingi na kuwafanya waishi katika umaskini wa kupindukia. Kupitia LSF, kwa kushirikiana na Wasaidizi wa Kisheria, inatoa msaada wa kisheria kwa wajane wanaokumbwa na changamoto hizi. Jitihada hizi zinahusisha: 1. Elimu ya haki za kisheria kwa wajane na jamii kwa ujumla. 2. Kusaidia kufungua kesi za kisheria ili wajane wapate haki zao za kumiliki ardhi na mali. 3. Kuwajengea uwezo wa kujitegemea kiuchumi kupitia programu za mafunzo na uwezeshaji. Kwa pamoja, tunapambana kuhakikisha kila mwanamke anapata haki zake na kuishi kwa heshima. #HakiKwaWajane #SautiYaMwanamke #TokomezaUkatiliWaKijinsia

  • View organization page for LSF, graphic

    1,435 followers

    Waziri wa Katiba na Sheria Dkt Damas Ndumbaro pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Kilombero Mhe. Dunstan Kyobya na Mkuu wa Wilaya ya Morogoro Mhe. Mussa Kilakala wakitoa huduma za Msaada wa Kisheria kwa Wananchi mbalimbali waliojitokeza katika Uzinduzi wa Kampeni ya Huduma za Msaada wa Kisheria Mkoani Morogoro.

    • No alternative text description for this image
  • View organization page for LSF, graphic

    1,435 followers

    Bwana Gabriel Ngoi, msaidizi wa kisheria kutoka Mvomero, akimweleza Waziri wa Katiba na Sheria, Dkt. Damas Ndumbaro, kuhusu kazi zinazofanywa na wasaidizi wa kisheria katika kutatua migogoro na kutoa elimu kwa jamii chini ya ufadhili wa LSF. Aidha, aliomba huduma hizi kuwa endelevu, kwani kwa mwaka wasaidizi wa kisheria hushughulikia migogoro zaidi ya 70,000, ambapo asilimia 73 ya migogoro hiyo hutatuliwa na wasaidizi hawa walioko nchi nzima.

    • No alternative text description for this image
  • View organization page for LSF, graphic

    1,435 followers

    LSF, ikiwa Makamu Mwenyekiti wa Kampeni ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia, imeshiriki kikamilifu katika uzinduzi rasmi wa Kampeni hiyo uliofanyika tarehe 13 Desemba 2024, Mkoani Morogoro, ukiongozwa na Waziri wa Katiba na Sheria, Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro. Kampeni hii inalenga kuongeza uelewa wa wananchi kuhusu haki zao za kisheria, kupunguza ukatili wa kijinsia, na kuhakikisha huduma za msaada wa kisheria zinapatikana kwa urahisi zaidi hasa kwa wanawake na watoto. Mafanikio yaliyopatikana tangu kuanzishwa kwa kampeni hii ni pamoja na: 1.Kuongezeka kwa idadi ya watu wanaotumia huduma za msaada wa kisheria. 2.Kupungua kwa migogoro ya kifamilia kupitia suluhisho la kisheria. 3.Kukuza ushirikiano baina ya wadau wa haki na jamii katika kusimamia haki kwa wote. LSF itaendelea kushirikiana na Serikali na wadau wengine kuhakikisha malengo ya Kampeni hii yanatimia na haki inawafikia wananchi wote, bila ubaguzi.

    • No alternative text description for this image
  • View organization page for LSF, graphic

    1,435 followers

    LSF tumeshiriki katika tukio la ugawaji tuzo kwa Vinara 16 wa Kupinga Ukatili wa Kijinsia mapema wiki hii. Vinara hawa ni mfano wa kuigwa katika jamii kwa juhudi zao za kusimama kidete dhidi ya ukatili wa kijinsia, kusaidia wahanga, na kuhamasisha mabadiliko chanya. Ushindi wao ni ushuhuda wa kwamba kila mmoja wetu ana nafasi ya kuleta tofauti kupitia elimu, uhamasishaji, na hatua za kijamii. Kuwahamasisha wengine kuwa vinara wa kupinga ukatili wa kijinsia ni njia muhimu ya kuhakikisha jamii inakuwa salama kwa kila mtu. Pamoja tunaweza kujenga kizazi kinachothamini usawa wa kijinsia na heshima kwa haki za binadamu. #TunzaUsawa #PingaUkatiliWaKijinsia

    • No alternative text description for this image
  • View organization page for LSF, graphic

    1,435 followers

    Today, we join the world in celebrating International Human Rights Day, reaffirming the importance of protecting and promoting the rights of all people. Through the Sauti ya Mwanamke project, LSF continues to champion women's and girls' rights by providing legal aid and raising awareness on human rights. Together, we can build a society that upholds equality and justice for everyone.

    • No alternative text description for this image
  • View organization page for LSF, graphic

    1,435 followers

    RUN FOR BINTI MARATHON YABORESHA ELIMU, AFYA NA MAZINGIRA MTWARA. Mbio za hisani za Run for Binti Marathon zimefanikiwa kuboresha mazingira ya Shule ya Sekondari Mnyawi, Mtwara, kwa kujenga vyoo vya kisasa vyenye matundu 12 na kugawa taulo za kike zinazotumika tena kwa zaidi ya wanafunzi 200. Pia, miti 100 imepandwa kwa ajili ya utunzaji wa mazingira. Wanafunzi na jamii walipatiwa elimu kuhusu ukatili wa kijinsia, hedhi salama, afya ya uzazi, elimu ya fedha, na nishati safi kupitia wadau kama Stanbic Bank, Marie Stopes, na Girl Guide Tanzania. Mkurugenzi wa Smile for Community, Bi Flora Njelekela, alieleza kuwa mbio hizi zimekuwa zikiboresha maisha ya wanafunzi na jamii kwa miaka mitatu mfululizo. Mgeni rasmi, Mkuu wa Wilaya ya Mtwara, Abdallah Mwaipaya, aliwashukuru wadau kwa mchango wao na kusisitiza umuhimu wa kutunza miundombinu na kupunguza changamoto za kijamii. Wadhamini wakuu wa mbio hizi walikuwa Stanbic Bank, Songas, East Africa Law Society, na Azam Media, huku washiriki zaidi ya 800 wakihamasishwa kuchangia maendeleo ya jamii. Maandalizi ya mbio za mwaka 2025 yameanza rasmi, zikilenga kuadhimisha Wiki ya Hedhi Salama.

    • No alternative text description for this image

Similar pages