Wakatari
Wakatari (kutoka neno la Kigiriki katharos, yaani safi) walikuwa Wakristo wa karne za kati waliofuata aina ya Gnosis ya kale iliyozidi kupatikana huko na huko, kwa mfano kati ya Wamani.
Mitazamo
[hariri | hariri chanzo]Waliamini ulimwengu umeumbwa na mungu mbaya na kwamba huyo alimnyang'anya Mungu mwema watu na kuwaleta ulimwenguni. Kumbe ndani ya mwili wao kuna roho inayohitaji kumrudia Mungu.
Walikataa mafundisho kuhusu dhambi, kumbe waliamini mtu akifa mungu mbaya anairudisha tena ulimwenguni katika mwili mwingine mpaka mtu afikie utakaso.
Walikubali Agano Jipya tu, wakitumia tafsiri za lugha za kawaida, si za Kilatini.
Pia walikataa ndoa, kunywa maziwa na kula nyama, isipokuwa samaki.
Lakini walidai kati yao waliokamilika tu wafuate maadili hayo, wakiwaachia waumini wengine wafanye walivyotaka hadi kutubu saa ya kufa.
Matatizo
[hariri | hariri chanzo]Mwaka 1145 walianza kushambulia Kanisa Katoliki, na kufikia mwaka 1165 walisema hadharani limejaa mbwamwitu wakali na wanafiki wanaoabudu mungu mwingine, si yule wa kweli.
Mwaka 1166 mtaguso wa Oxford uliwafuta Wakatari wa huko Uingereza. Ikatokea vilevile Ufaransa Kaskazini.
Hivyo mwaka 1167 maaskofu Wakatari walikutana ili kuanzisha kanisa mbadala huko Ufaransa Kusini, walipokuwa wanaungwa mkono na watawala wadogo.
Maitikio
[hariri | hariri chanzo]Kanisa Katoliki, ingawa mapadri wake hawakuwa na maadili mazuri, lilipinga Ukatari kama uzushi. Hata hivyo ulizidi kuenea katika mazingira ya juhudi kubwa ya mijini, wakati Wakatoliki walizidi kuwa na nguvu mashambani, kwenye monasteri.
Hatimaye Papa aliagiza vita vya msalaba dhihi yao akiwaahidia askari wote fadhili zilezile walizopewa waliokwenda kupigana na Waislamu.
Tarehe 22 Julai 1209 askari 30,000 hivi waliteka Beziers na kuua wakazi wote (labda 20,000), wengi wao wakiwa Wakatoliki. Vita viliendelea miaka arubaini hivi, kwa lengo la kukomesha Wakatari wote Ufaransa Kusini.
Mwaka 1210 walianza kuchoma moto watu hai, desturi iliyoendelea kwa wazushi wengine baadaye.
Katika miji ya Italia Kaskazini Ukatari ulikoma miaka ya 1260. Guillaume Bélibaste, "mkamilifu" wa mwisho wa Languedoc, aliuawa mwaka 1321.
Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]- http://dannyreviews.com/h/Cathars.html
- http://gnosistraditions.faithweb.com/mont.html
- http://www.fordham.edu/halsall/source/gui-cathars.html Ilihifadhiwa 4 Oktoba 2003 kwenye Wayback Machine.
- http://philtar.ucsm.ac.uk/encyclopedia/ Ilihifadhiwa 13 Oktoba 2007 kwenye Wayback Machine. christ/west/cathar.html
- http://pages.britishlibrary.net/forrester-roberts/ Ilihifadhiwa 4 Oktoba 2003 kwenye Wayback Machine. cathars.html
- http://www.rennes-le-chateau.co.uk/html/cathars.htm
- Cathar Center in Barcelona: Books, spirituality, exhibition Ilihifadhiwa 12 Septemba 2009 kwenye Wayback Machine.
Makala hii kuhusu dini ya Ukristo bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Wakatari kama historia yake, matokeo au athari zake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |