Nenda kwa yaliyomo

Shilo

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Sinagogi la Mishkan Shilo lililojengwa Shilo kwa kuiga hekalu lake la zamani.

Shilo ulikuwa mji wa zamani unaotajwa katika Biblia ya Kiebrania, karibu na Khirbet Seilun, kusini kwa Tirza.[1]

Ulikuwa makao ya hekalu lilipotunzwa sanduku la agano kabla ya hilo kutekwa na Wafilisti wakati wa kuhani Eli na hatimaye kuhamishiwa na mfalme Daudi mjini Yerusalemu, ambapo mwanae Solomoni alilijengea hekalu la fahari.

Nabii Yeremia alichukua Shilo kama kielelezo cha maangamizi yatakayolipata hekalu la Yerusalemu kutokana na Waisraeli kutokubali ujumbe wa toba aliowaletea kutoka kwa Mungu.

  1. "Shiloh, Israel's Capital for 400 Years, Being Uncovered," Gil Ronen, July 28, 2010, Jerusalem Post.
  • Finkelstein, Israel, et al. Shiloh: The Archaeology of a Biblical City. Tel Aviv, 1993.

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]
Wikimedia Commons ina media kuhusu:

shilo unaweza ifananisha na makkha kwa tukio zima japo tofaut ni kwmba makkha kuna kaburi la mtume s.w.a na shilo lipo sanduku la agano

Makala hii kuhusu eneo fulani bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu eneo hilo kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Je, unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.


Usitaje majina ya madiwani na viongozi au maafisa wengine wa sasa maana wanabadilika haraka mno.