Oppland
Oppland ilikuwa moja kati ya Majimbo ya Norwei. Jimbo lilipakana na Sør-Trøndelag, Møre og Romsdal, Sogn og Fjordane, Buskerud, Akershus, Oslo na Hedmark. Ngazi ya utawala ya jimboni hapa ilikuwa mjini Lillehammer. Oppland pamoja na Hedmark ilikuwa moja kati ya majimbo pekee yaliyozungukwa na bandari nchini Norwei.
Jiografia
[hariri | hariri chanzo]Oppland ilienea kutoka maziwa Mjøsa na Randsfjorden hadi kuelekea katika milima ya Dovrefjell, Jotunheimen na Rondane. Jimbo hili liligawanyika katika wilaya za zamani, ambazo ni Gudbrandsdalen, Valdres, Toten, Hadeland na Land.
Oppland ukubwa wake ulimujumuisha miji ya Lillehammer, Gjøvik, Otta na Fagernes, na milima miwili mirefu sana ya Norwei, ambayo ni Glittertind na Galdhøpiggen.
Kuna majumba ya makumbusho kadhaa na vivutio vingine vilivyopo mjini Oppland na utalii ni pato muhimu sana kwa uchumi, Valdres na Gudbrandsdal huwa miongoni mwa vivutio mashuhuri sana. Gudbrandsdal imezunguka mto Gudbrandsdalslågen, na ina vijiji kama vile Øyer, Dovre na Dombås. Valdres inajumuisha eneo linaloanzia kutoka Jotunheimen hadi Bagn katika mto Begna. Ni sehemu mashuhuri sana kwa mchezo wa skiing na michezo mingine ya kipindi cha baridi. Mahali ambapo kuna wakazi wengi katika jimbo hili ni Beitostølen na Fagernes.
Kwa sasa imeunganishwa na Hedmark kuunda jimbo jipya la Innlandet.
Manispaa
[hariri | hariri chanzo]Jimbo la Oppland lilikuwa na jumla ya manispaa 26:
Viungo vya Nje
[hariri | hariri chanzo]- media kuhusu Oppland pa Wikimedia Commons
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]Makala hii kuhusu maeneo ya Norwei bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Oppland kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |