Keebler (kampuni)
Kampuni ya Keebler ni kampuni ya pili kwa ukubwa ya kuzalisha kuki katika nchi ya Marekani.
Ilianzishwa katika mwaka wa 1853, imezalisha baadhi ya vitafunio vingi sana vya kuokwa. Keebler inauza bidhaa kama:
- Cheez-Its(ambayo ina nembo ya Sunshine Biscuits)
- Chips Deluxe,
- Club Crackers,
- EL Fudge Cookies,
- Famous Amos Cookies,
- Fudge Shoppe Cookies,
- Murray,
- Austin, Plantation,
- Vienna Fingers,
- Town House Crackers ,
- Wheatables,
- Sandie's Shortbread,
- Zesta Crackers, miongoni mwa zingine.
Kaulimbiu ya Keebler ni "Uncommonly Good" ikimaanisha nzuri sana kawa nji isiyoya kawaida. Tom Shutter na Leo Burnett ndio walioandika wimbo wa matangazo ya Keebler unaojulikana sana.
Historia ya Kampuni
[hariri | hariri chanzo]Godfrey Keebler alianza kwa kufungua jumba la kuoka mjini Philadelphia,Pennyslvania katika mwaka wa 1853. Katika mwaka wa 1927,jumba hilo la uokaji na mengine yaliyoundwa na Kampuni ya United Biscuits, ambayo ilikuwa,wakati fulani, na makao yake makuu West Drayton, Middlesex, Uingereza.
Jumba la uokaji la Keebler-Wyl likawa mwokaji rasmi wa kuki za Girl Scout Cookie katika mwaka wa 1936, ikawa kampuni ya kwanza ya kibiashara iliyooka biskuti hizo(hapo awali wanaskauti na akina mama ndio waliooka kuki hizo). Ilipofika mwaka wa 1978,kampuni nne zilikuwa zikioka kuki hizi. Little Brownie Bakers ndiyo sehemu ya Keebler iliyo na kibali cha kutayarsha kuki hizo.
Katika mwezi wa Machi 2001,Kampuni ya Keebler ilinunuliwa na kampuni ya Kellog. Wakati huo, makao yao makuu yalikuwa mjini Elmhurst,katika eneo la Illinois. [5]
Keebler Elves
[hariri | hariri chanzo]Katuni za Keebler Elves,wakiongozwa na Ernest J. Keebler au Ernie,wanajulikana sana katika katuni za matangazo. Katuni hizi zilihusishwa katika matangazo mengi ya televisheni katika miaka iliyopita zikionyeshwa zikioka bidhaa mbalimbali. Nembo ya Keebler ya mti inaonyesha katuni hizi.
Kampuni ya Burnett iliunda katuni hizo katika mwaka wa 1968,wakiita jumba la uokaji la katuni hizo:The Hollow Tree Factory.
JJ Keebler ndiye aliyekuwa katuni mkuu katika mwaka wa 1969. Ernie Keebler akawa katuni mkuu katika mwaka wa 1970. [9] Ernie ana nywele nyeupe,koti ya kijani kibichi,shati nyeupe,tai ya manjano na viatu vikubwa.
Katuni zingine zilikuwa:Fryer Tuck (ambaye alihusishwa na "Munch-ems"), Zoot na JJ (wanaajulikana sana kwa Pizzarias), mama yake Ernie- Ma Keebler,Elmer Keebler,Buckets (ambaye hutupa chokoleti kwenye kuki),Fast Eddie (ambaye hupakia bidhaa ),Sam (muundaji wa siagi ya njugu),Roger (muuzaji wa mapambio),Doc (daktari na mwokaji wa kuki),Zack (msimamizi wa duka ),Flo (mhasibu), Leonardo (msanii), Elwood , Profesa, Edison, Larry na Art.
Nembo ya The Hollow Tree ilirudiwa katika viwanda vya Keebler na Kellog katika Columbus,Georgia na Elmhurst,Illinois ambavyo barabara zao ziaitwa 1 Hollow Tree Lane.
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- http://www.brilliant-marketing.com/products/index.php?cPath=22 Ilihifadhiwa 2 Aprili 2010 kwenye Wayback Machine.,
- http://www.tvacres.com/admascots_keebler.htm Archived 2012-09-13 at Archive.today,
- http://www.pabook.libraries.psu.edu/palitmap/GirlScoutCookies.html Ilihifadhiwa 10 Juni 2010 kwenye Wayback Machine.,
- http://www.illinois.com/details/city.php?cityFips=1723620 Ilihifadhiwa 3 Septemba 2009 kwenye Wayback Machine.,