Nenda kwa yaliyomo

Fungo-miti wa Afrika

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Fungo-miti
Fungo-miti (Nandinia binotata)
Fungo-miti (Nandinia binotata)
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Chordata (Wanyama wenye ugwe wa neva mgongoni)
Ngeli: Mammalia (Wanyama wenye viwele wanaonyonyesha wadogo wao)
Oda: Carnivora (Wanyama mbua)
Nusuoda: Feliformia (Wanyama kama paka)
Familia: Nandiniidae (Wanyama walio na mnasaba na paka-zabadi)
Pocock, 1929
Jenasi: Nandinia
Gray, 1843
Spishi: N. binotata
(Gray, 1830)
Uenezi wa fungo-miti
Uenezi wa fungo-miti

Fungo-miti (wa Afrika) (jina la kisayansi: Nandinia binotata) ni mnyama mbuai mdogo, spishi pekee ya jenasi yake na ya familia yake Nandiniidae[1]. Hii ni spishi ya misitu mizito ya Afrika ambapo huishi mitini. Mnyama huyu ni mpweke na hukiakia usiku.

Ana mwili ufananao na ule wa paka mdogo wenye miguu mifupi, masikio madogo na mkia wa urefu uleule wa mwili. Wanyama wazima huwa na uzito wa kg 1.7 hadi 2.1.

Hula vitu vyingi kama wagugunaji, wadudu, mayai, mizoga, matunda, ndege na popo-matunda. Fungo-miti ni mnyama ambaye hula sana bila kujali kesho. Hulka ya kula kwake imeleta msemo "Unakula sana kama Fungo" Ni nadra kuona kinyesi chake maana huwa na sehemu moja ya kuendea choo kama vile paka, pia njia anayoitumia ni moja tu.

Ijapo fungo-miti anafanana na spishi za fungo za familia Viverridae, inaonekana ni tofauti kinasaba na aliachana na fungo kabla ya paka. Kwa hiyo amepewa jenasi na familia yake binafsi, lakini kuna wataalamu ambao hawakubali.

  1. Wozencraft, W. Christopher (2005). "Order Carnivora (pp. 532-628)". In Wilson, Don E., and Reeder, DeeAnn M., eds. Mammal Species of the World: A Taxonomic and Geographic Reference (3rd ed.). Baltimore: Johns Hopkins University Press, 2 vols. (2142 pp.). ISBN 978-0-8018-8221-0.

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Makala hii kuhusu mnyama fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Fungo-miti wa Afrika kama uainishaji wake wa kibiolojia, maisha au uenezi wake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.