Dr. Dre Presents: The Aftermath ni albamu ya kompilesheni ambayo imetolewa na kutayarishwa na rapa na mtayarishaji wa Kimarekani, Dr. Dre. Albamu ilitolewa mnamo tar. 26 Novemba, 1996, wiki moja baada ya kutolewa kibao chake kikuu cha "East Coast, West Coast, Killas" akiwa na Group Therapy. Albamu hii ilikuwa ya kwanza ya Dre baada ya kuondoka Death Row Records, na lilikuwa toleo lake la kwanza tangu kuanzishwa kwa studio yake mpya iliyokwenda kwa jina la Aftermath Entertainment.
Licha ya jina la Dr. Dre kuwa katika albamu, na kutunukiwa platinum,[1] imepokea tahakiki mchanganyiko na haikuwa miongoni mwa matoleo ya mwaka yenye mafanikio makubwa kibiashara. Baadaye albamu ilifuatiwa na kibao chake cha pili kilichoimbwa na Dr. Dre peke yake "Been There, Done That".
↑[Dr. Dre Presents the Aftermath katika Allmusic allmusic ((( Dr. Dre Presents...The Aftermath > Charts & Awards > Billboard Albums )))]. Allmusic. Imeingizwa Mei 29, 2008.