Anastasia wa Sirmio
Mandhari
Anastasia wa Sirmio (kwa Kigiriki: Ἁγία Ἀναστασία ἡ Φαρμακολύτρια[1]; alifariki Sirmium, leo nchini Korasya, 25 Desemba 304 [2]) alikuwa mwanamke Mkristo aliyeuawa kwa sababu ya imani yake katika dhuluma ya kaisari Dioklesyano[3].
Ndiyo maana anaheshimiwa tangu zamani na Wakatoliki, Waorthodoksi na Waorthodoksi wa Mashariki kama mtakatifu mfiadini.
Sikukuu yake inaadhimishwa ama tarehe 22 Desemba ama 25 Desemba[4] ama 26 Desemba.
Maisha na heshima baada ya kifo
[hariri | hariri chanzo]Inasemekana wazazi wake walikuwa Praetextatus na Fausta wa Sirmio na Krisogoni alikuwa mlezi wake.
Masalia yake yanatunzwa katika Kanisa kuu la Zadar, Kroatia.
Ni kati ya wanawake saba ambao, mbali ya Bikira Maria, wanatajwa katika Kanuni ya Kirumi ya Misa.
Tazama pia
[hariri | hariri chanzo]- Watakatifu wa Agano la Kale
- Orodha ya Watakatifu Wakristo
- Orodha ya Watakatifu wa Afrika
- Orodha ya Watakatifu Wafransisko
Tanbihi
[hariri | hariri chanzo]- ↑ "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2018-02-25. Iliwekwa mnamo 2019-04-26.
- ↑ https://www.santiebeati.it/dettaglio/83175
- ↑ Smith, Philip (1867). "Anastasia". Katika William Smith (mhr.). Dictionary of Greek and Roman Biography and Mythology. Juz. la 1. Boston: Little, Brown and Company. uk. 158.
- ↑ Martyrologium Romanum
Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]Wikimedia Commons ina media kuhusu:
- Catholic Encyclopedia: St. Anastasia
- Patron Saints: Anastasia
- Greatmartyr Anastasia the "Deliverer from Potions" Orthodox Synaxarion and icon of the saint
- "Saint Anastasia" at the Christian Iconography website
- "Historia de Sancta Anastasia" (in Latin), from Jacobus de Voragine, Legenda Aurea.
- Translation Ilihifadhiwa 5 Mei 2019 kwenye Wayback Machine. of the above, by Richard Stracke
Makala hii bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari. |