Nenda kwa yaliyomo

24 (msimu wa 6)

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Msimu wa 6 wa 24

Season 6 Cast
Nchi asilia Marekani
Mtandao Fox Broadcasting Company
Iko hewani tangu 14 Januari 2007 – 21 Mei 2007
Idadi ya sehemu 24
Msimu uliopita Msimu wa 5
Msimu ujao Msimu wa 7

Msimu wa Sita (pia unajulikana kama Siku ya 6) ya mfululizo wa televisheni wa 24 ulioanza kurushwa hewani nchini Marekani mnamo siku ya Jumapili, 14 Januari 2007, Uingereza mnamo 21 Januari 2007 na nchini Australia mnamo 30 Januari 2007.

Hadithi ya msimu huu inaanza na kuisha saa 12:00 asubuhi. Ni seti ya miezi 20 baada ya matukio ya msimu wa tano.

Muhtasari wa msimu

[hariri | hariri chanzo]

Msimu wa Sita (2007) ni seti ya miezi 20 (Mei 2011) baada ya Msimu wa Tano. Wasanifu wa onyesho walieleza kwamba waliepuka matumizi ya tarehe ili kuacha mchezo "uende na wakati."[1]

Baada ya matukio ya Msimu wa Tano na zaidi ya majuma 11 ya kabla ya Siku ya 6, nchi ya Marekani ililengwa pwani-hadi-pwani na mfululizo wa wanaojiotoa mhanga na mabomu. Mtu mmoja aitwaye Abu Fayed amekubali kuwapa Marekani mahali pa gaidi Hamri Al-Assad, gadi anayedhaniwa kuwa ndiye muhusika mkuu wa mashambulizi hayo, kwa kubadilishana na kachero wa zamani wa CTU Jack Bauer ambaye alikuwa na ugomvi naye binafsi. Kwa kufuatia hilo, Rais Wayne Palmer akafanya mpango wa kutolewa kwa Bauer, ambaye alikamatwa kiharamu na Makachero wa Serikala ya China mwishoni mwa Siku ya 5, kwa makubaliano ya fedha nyingi mno.

Hata hivyo, wakati anapata mateso kutoka kwa Fayed, Bauer akagundua kwamba Assad ndiye hasa anayetaka kuzuia mashambulizi, na Fayed ndiye muhusika mkuu. Kwa bahati nzuri, Jack akaweza kutoroka, na kwenda kumwokoa Assad asije akauawa na shambulio la anga lililokuwa likitolewa na serikali yake. Jack na CTU, na msaada wa Assad, wakaweza kugundua nia ya kweli ya Fayed: kulipua bomu la nyuklia katika nchi ya Marekani. Baada ya shambulio moja la nyuklia, Jack ana kazi ya kutafuta uhueni wa mabomu ya nyuklia yaliyosalia, hivyo kupanga mfululizo wa matukio ya siku.

Wahusika

[hariri | hariri chanzo]

Hii ni orodha ya wahusika wakuu wa Msimu wa 6. Tazama orodha ya wahusika wa 24 kwa orodha iliyokamilika kabisa.

Nyota

Nyota Waalikwa Wageni

Wanajirudia

  1. Fienberg, Daniel (17 Januari 2007). "Looking for clues on the set of '24'". Zap2It.com. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2009-07-31. Iliwekwa mnamo 2009-07-31.

Viungo vy Nje

[hariri | hariri chanzo]