Nenda kwa yaliyomo

Lama

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Pitio kulingana na tarehe 13:45, 14 Machi 2014 na Kipala (majadiliano | michango)
(tofauti) ← Pitio lililotangulia | Toleo la sasa (tofauti) | Pitio linalofuata → (tofauti)

Kwa wanyama wenye jina hili tazama Lama (mnyama)

Lama (kitibeti: བླ་མ་; Wylie: bla-ma) ni cheo cha heshima kwa mwalimu wa kidini wa Tibet. Jina hili linafanana na lile la kisanskriti 'guru' (taz. Ubuddha wa kitibeti na Bön).

Ni cheo kinachoweza kutumika kama tunuko kwa mtawa wa kike au wa kiume au (katika shule za Nyingma, Kagyu na Sakya) wanaojihusisha na kufanya mambo ya kitantra waliosonga kusudi kuwapa sifa ya kuweza kufundisha na mamlaka ya kufanya hivyo kulingana na ngazi waliyofikia; au wanaweza kuwa sehemu ya cheo kama Dalai Lama ama Panchen Lama kama itumikavyo kwa koo za malama wenye kuzaliwa tena (Tulkus).