Nenda kwa yaliyomo

Catherine Denguiadé

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Pitio kulingana na tarehe 14:18, 22 Aprili 2024 na Praygod mwanga (majadiliano | michango)
(tofauti) ← Pitio lililotangulia | Toleo la sasa (tofauti) | Pitio linalofuata → (tofauti)
Catherine Martine Denguiadé

Muhuri wa mwaka 1978 ukikumbuka maadhimisho ya kumbukumbu ya mwaka mmoja wa Ufalme wa Bokassa.
Amezaliwa 7 Agosti 1949
Sarh, Chad
Nchi Chad


Catherine Martine Denguiadé, ambaye pia anajulikana kama Catherine Bokassa (alizaliwa 7 Agosti 1949), ni mwanachama wa zamani wa familia ya kifalme wa Afrika ya Kati na mjane wa Jean-Bédel Bokassa. Alikuwa mmoja wa wake kadhaa wa Kaisari Bokassa lakini akawa Malkia alipounda ufalme wa Afrika ya Kati. Mtoto wake wa kiume alichaguliwa kama mrithi wake.

Denguiadé alizaliwa huko Sarh nchini Chad. Baba yake alitoka CAR lakini mama yake alitoka Chad na hapo ndipo alipoanza elimu yake. Elimu yake ya sekondari alipata huko Bangui.

Aliolewa akiwa na umri wa miaka kumi na minne. Alikamatwa na Bokassa ili awe mke wake wa tatu. Baadaye aliowa wanawake wengine kumi na wanne.[1]

Alikuwa mshiriki kwa njia fulani wa tukio hilo mwaka 1977 wakati kipindi cha mume wake cha kushuka kwa nguvu kilipoanza. Aliitoa amri kusema kuwa kila mtoto anayehudhuria shule katika ufalme wake anapaswa kuvaa sare ya shule. Ilionekana baadaye kwamba Denguiadé alikuwa mmiliki wa kampuni iliyotengeneza sare hizo.[2] Mwezi Disemba 1977, mumewe alijitangaza kuwa Kaisari wa Afrika ya Kati na Jamhuri ya Afrika ya Kati ikawa Ufalme wa Afrika ya Kati. Aliamua kumtawaza Catherine kuwa Malkia Mke na alikuwa amevaa mavazi kutoka kampuni ya mitindo ya Kifaransa ya Lanvin. Vitu vingi vya kifahari vilivyohitajika kwa tukio la kutawazwa vililetwa kutoka Ufaransa. Rais wa Ufaransa alituma farasi wanane kutoka Normandy kuvuta gari lao la kifahari. Katika tukio hilo, farasi wawili walikufa na wawili hao walilazimika kutumia gari.[1] Mwanae wakiume wa miaka minne Jean-Bédel Bokassa Jr. alihudhuria sherehe hiyo akiwa mtoto wa mrithi. Alikuwa ametajwa kuwa mrithi (prince héritier de Centrafrique). Mwanae alikuwa na ndugu wakubwa na ndugu wa kambo. Mmoja wa ndugu wa kambo wa mwanae, Georges aliteuliwa kuwa waziri wa baraza lakini mumewe alisema hakuwa na nguvu za kutosha kuwa mrithi.[3]

Mwaka 1979 alikuwa Geneva akiishi uhamishoni na watoto wake saba pamoja na aliyekuwa mfalme. Inasemekana aliuza almasi kila alipokuwa hana pesa za kutosha.[1]

Baada ya Bokassa kufariki, alipata msaada kutoka kwa marafiki. Kadri muda ulivyopita, yeye pamoja na watoto wake walirejea Jamhuri ya Afrika ya Kati.


  1. 1.0 1.1 1.2 Marlowe, Lara. "The Central African Republic, where Emperor Bokassa ruled with violence and greed". The Irish Times (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2021-01-29.
  2. "The Exile Factor: Wives of Deposed Dictators". The Independent (kwa Kiingereza). 2011-10-23. Iliwekwa mnamo 2021-01-29.
  3. Titley, Brian (1997) Dark Age: The Political Odyssey of Emperor Bokassa, McGill-Queen's University Press, ISBN 0-7735-1602-6, pp. 86–87
Makala hii kuhusu mwanasiasa fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Catherine Denguiadé kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.