Nenda kwa yaliyomo

Mary I wa Uingereza

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Pitio kulingana na tarehe 14:32, 11 Februari 2023 na Riccardo Riccioni (majadiliano | michango) (Masahihisho aliyefanya InternetBuddy2 (Majadiliano) yalirejeshwa hadi sahihisho la mwisho na Riccardo Riccioni)
(tofauti) ← Pitio lililotangulia | Toleo la sasa (tofauti) | Pitio linalofuata → (tofauti)
Malkia Mary I.

Mary I wa Uingereza (pia anajulikana kama Mary Tudor na kama "Bloody Mary"; 18 Februari 1516 - 17 Novemba 1558) alikuwa Malkia wa Uingereza na Ireland kutoka Julai 1553 hadi kifo chake mwaka wa 1558.

Anajulikana hasa kwa jaribio lake la kubadili Matengenezo ya Kiingereza ambayo yalikuwa yameanza wakati wa utawala wa baba yake, Henry VIII na kurudisha nchi chini ya Kanisa Katoliki. Jaribio lake la kurejesha kwa Kanisa mali iliyotwaliwa na wafalme wawili waliopita lilizuiwa kwa kiasi kikubwa na Bunge la Uingereza. Lakini wakati wa utawala wake wa miaka mitano, Mary aliagiza kesi dhidi ya wapinzani wa Ukatoliki zaidi ya 280 waliochomwa motoni wakiwa hai kama wazushi.

Mary alikuwa mtoto wa Henry VIII na mke wake wa kwanza, Katarina wa Aragon, ambaye peke yake kati ya watoto wa tumbo moja aliishi hadi kuwa mtu mzima. Alirithi ufalme baada ya kifo cha ndugu yake mdogo Edward VI, aliyezaliwa na Henry VIII na mke wake wa tatu, Jane Seymour.

Baada ya kifo cha Mary kwenye mwaka 1558, hatua zake za kurudisha Ukatoliki katika Uingereza zilibatilshwa na mdogo wake na mrithi, Elizabeth I, aliyezaliwa na Henry VIII na mke wake wa pili, Anne Boleyn.

WikiMedia Commons
WikiMedia Commons
Wikiquote ina mkusanyiko wa dondoo kuhusu:
  • "Mary I (1516–1558)". BBC.
Makala hii kuhusu mwanasiasa fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mary I wa Uingereza kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.