Joseph Makama Kusaga : Tofauti kati ya masahihisho
d →WASIFU WA JOSEPH MAKAMA KUSAGA: kuongeza taarifa |
d →Maisha ya udogoni na elimu yake: kuongeza taarifa Tags: KihaririOneshi Disambiguation links |
||
Mstari 5: | Mstari 5: | ||
==Maisha ya udogoni na elimu yake== |
|||
Katika familia ya watoto 9 wa mzee Kusaga (wa kabila la [[Wakurya]]), Joe ni wa nne. Aliondoka [[Musoma]] na kuhamia [[Dar Es Salaam]] akiwa na umri wa miaka mitano kufuatia kuhamishwa kwa baba yake ambaye alikuwa mtumishi wa umma.<ref> https://www.jamiiforums.com/threads/historia-ya-joseph-kusaga.1748466/</ref> Aliendelea na masomo akiwa Dar katika shule za [msingi na sekondari] [[Muhimbili]], [[Forodhani]] na [[Mzizima]]. Katika ngazi ya elimu ya juu, alisomea uhandisi wa umeme.<ref>https://tanzania.mom-gmr.org/en/owners/individual-owners/detail/owner/owner/show/joseph-m-kusaga/</ref> |
|||
Kabla ya kuibuka na kuwa Joe anayefahamika hivi sasa, kichocheo cha awali kilikuwa kupenda kwake sana [[muziki]] na burudani wakati akisoma shule. Hali hiyo ilitanabaisha ukweli kuwa Joe alikuwa "upande wa mwenge wa shilingi" na baba yake alikuwa upande wa "kichwa" (Baba yake alipenda muziki na burudani sawa na Joe). |
|||
Kuanza kwake kuendesha shughuli za muziki na burudani katika umri mdogo huku akiwa chuoni, kulikubaliwa na wazazi wake japo kwa tahadhari. Walikuwa ni aina ya wazazi wasaidiao kufanikisha ndoto za mtoto.<ref>https://tanzania.mom-gmr.org/en/owners/companies/detail/company/company/show/clouds-entertainment-co-limited-1/</ref> Katika jitihada zake za mwanzo kabisa za kuendesha discotheques na boogies (matamasha ya muziki ya muda wa mchana), Joe alifuga kuku kujipati mtaji na aliazima vifaa vya kielektroniki vya familia. |
|||
Kutokana na kipaji na kukubalika kwake kama Dj na mpanga matamasha, Joe alipata mafanikio makubwa. Alifanya matamasha kwenye kumbi zote maarufu za Dar na mashabiki walimpachika majina kuashiria kuwa yeye ni [[mfalme]] wa [[tasnia]]. Baada ya mafanikio hayo, akajiwa na wazo la kufanya ziara [[Marekani|nchini Marekani]]. Huko ndiko alikopata wazo la kuanzisha kituo cha [[redio]] kadhalika alikutana na rafikiye wa kuliana yamini, Ruge Mutahaba.<ref> https://www.jamiiforums.com/threads/historia-ya-joseph-kusaga.1748466/</ref> <ref>https://tanzania.mom-gmr.org/en/owners/companies/detail/company/company/show/clouds-entertainment-co-limited-1/</ref> |
|||
<references><nowiki>==Kampuni na miradi==</nowiki></references> |
Pitio la 00:29, 14 Desemba 2024
WASIFU WA JOSEPH MAKAMA KUSAGA
Joseph Makama Kusaga (alizaliwa Juni 9, 1966 mkoani Mara, Tanzania) maarufu kwa majina ya Big Joe, Biggy na Boss Joe, ni mwekezaji wa kitanzania mwenye maono ya kupigiwa mfano ya ujasiriamali wa kikampuni, anayefahamika kwa uasisi wake wa Clouds Entertainment Limited (sasa Clouds Media Group) kwa kushirikiana na aliyekuwa mbia na rafiki yake mkubwa, hyt. Ruge Mutahaba. [1] [2]
Katika familia ya watoto 9 wa mzee Kusaga (wa kabila la Wakurya), Joe ni wa nne. Aliondoka Musoma na kuhamia Dar Es Salaam akiwa na umri wa miaka mitano kufuatia kuhamishwa kwa baba yake ambaye alikuwa mtumishi wa umma.[3] Aliendelea na masomo akiwa Dar katika shule za [msingi na sekondari] Muhimbili, Forodhani na Mzizima. Katika ngazi ya elimu ya juu, alisomea uhandisi wa umeme.[4]
Kabla ya kuibuka na kuwa Joe anayefahamika hivi sasa, kichocheo cha awali kilikuwa kupenda kwake sana muziki na burudani wakati akisoma shule. Hali hiyo ilitanabaisha ukweli kuwa Joe alikuwa "upande wa mwenge wa shilingi" na baba yake alikuwa upande wa "kichwa" (Baba yake alipenda muziki na burudani sawa na Joe).
Kuanza kwake kuendesha shughuli za muziki na burudani katika umri mdogo huku akiwa chuoni, kulikubaliwa na wazazi wake japo kwa tahadhari. Walikuwa ni aina ya wazazi wasaidiao kufanikisha ndoto za mtoto.[5] Katika jitihada zake za mwanzo kabisa za kuendesha discotheques na boogies (matamasha ya muziki ya muda wa mchana), Joe alifuga kuku kujipati mtaji na aliazima vifaa vya kielektroniki vya familia.
Kutokana na kipaji na kukubalika kwake kama Dj na mpanga matamasha, Joe alipata mafanikio makubwa. Alifanya matamasha kwenye kumbi zote maarufu za Dar na mashabiki walimpachika majina kuashiria kuwa yeye ni mfalme wa tasnia. Baada ya mafanikio hayo, akajiwa na wazo la kufanya ziara nchini Marekani. Huko ndiko alikopata wazo la kuanzisha kituo cha redio kadhalika alikutana na rafikiye wa kuliana yamini, Ruge Mutahaba.[6] [7]
- ↑ https://www.jamiiforums.com/threads/historia-ya-joseph-kusaga.1748466/
- ↑ https://www.jifunzeujasiriamali.co.tz/2019/03/siri-kubwa-2-za-mafanikio-ya-ruge.html
- ↑ https://www.jamiiforums.com/threads/historia-ya-joseph-kusaga.1748466/
- ↑ https://tanzania.mom-gmr.org/en/owners/individual-owners/detail/owner/owner/show/joseph-m-kusaga/
- ↑ https://tanzania.mom-gmr.org/en/owners/companies/detail/company/company/show/clouds-entertainment-co-limited-1/
- ↑ https://www.jamiiforums.com/threads/historia-ya-joseph-kusaga.1748466/
- ↑ https://tanzania.mom-gmr.org/en/owners/companies/detail/company/company/show/clouds-entertainment-co-limited-1/