Gobori
Gobori ni silaha ya moto asilia. Ni aina ya bunduki ya msingi ambayo risasi pamoja na baruti zinaingizwa pamoja kwenye mdomo wa kasiba ya silaha na risasi inafyatuliwa kwa kupasha moto kwenye shimo upande wa nyuma ya kasiba. Moto inawasha baruti na kusababisha mlipuko unaorusha risasi nje ya mdomo wa kasiba. Bunduki za kisasa hutumia ramia zinazopelekwa katika kasiba kutoka kando au nyuma.
Hadi leo kuna aina kadhaa za mizinga zinazojazwa ramia kupitia mdomoni kama gobori. Vinginevyo gobori siku hizi ni silaha inayotumiwa kwa michezo au kutengenezwa na watu nyumbani kwa uwindaji haramu.
Kijeshi silaha hizo hazitumiwi tena tangu karne ya 19 kwa sababu matumizi yake ni ya polepole kulingana na bunduki za kisasa. Gobori inaweza kupigwa mara 1-2 kwa dakika, si haraka zaidi kama askari ameandaa tayari mizigo midogo ya baruti tayari kwa kila safari ya kupiga. Bunduki zinazotumia ramia zinaweza kupiga mara nyingi kwa dakika.
Tazama pia
haririViungo vya nje
hariri- National Muzzle Loading Rifle Association
- Muzzle Loaders association of Great Britain
- Detailed information on shooting muzzle loading pistols Archived 6 Julai 2010 at the Wayback Machine.
- Modern Muzzle Loading Misconceptions Archived 8 Julai 2011 at the Wayback Machine.
- Muzzle-Loading Associations International Committee