Idit Harel
Idit R. Harel (alizaliwa na kujulikana kama Idit Ron; Septemba 18, 1958) ni raia wa Marekani mwenye asili ya Israel, mjasiriamali na mwanzilishi wa kampuni inayojulikana kama Globaloria. Yeye ni mtafiti wa sayansi za kujifunza, na mwanzilishi wa makala zinazohusu mageuzi ya mbinu za kujifunza tangu mwanzo wa enzi ya teknolojia.
Jinsia | mwanamke |
---|---|
Nchi ya uraia | Israel |
Tarehe ya kuzaliwa | 18 Septemba 1958 |
Mahali alipozaliwa | Tel Aviv |
Kazi | educational psychologist |
Alisoma | Chuo Kikuu cha Harvard, Chuo cha Teknolojia cha Massachusetts, Tel Aviv University, Harvard Graduate School of Education |
Harel anatafiti na kuandika juu ya athari za teknolojia mpya ya kikokotozi ya vyombo vya habari kwenye maendeleo ya kijamii na kitaaluma ya watoto na epistemolojia yao. Utafiti wake wa ndani ya maabara ya MIT akiwa Seymour Papert umechangia katika ukuzaji wa nadharia ya ujifunzaji. Yeye huariri katika blogi yake kila mwezi kuhusu Teknolojia na kuhusu elimu ya ujuzi wa kompyuta, hasa kwa wanawake, wasichana, na watoto wasiojiweza, na thamani ya kozi kubwa za mtandaoni (MOOCs[1]) katika mageuzi ya elimu[2].
Maisha binafsi
haririIdit Ron alizaliwa huko Tel Aviv, nchini Israel. Wazazi wake na familia yao ni waathirika wa mauaji ya kimbari ya Wayahudi wa Ulaya wakati wa Vita vya pili vya dunia (1941 - 1945) kutoka Poland na Czechoslovakia. Aliolewa na mume wake wa kwanza, David Harel, mwaka 1979 (talaka 1995); wana watoto watatu. Aliolewa na mume wake wa pili, gavana wa zamani wa Virginia ya Magharibi, Gaston Caperton, mnamo mwaka 2003, na kuachana mwaka wa 2012[3].
Marejeo
hariri- ↑ Mooc.org. "MOOC.org | Massive Open Online Courses | An edX Site". www.mooc.org (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2022-11-25.
- ↑ "HuffPost - Breaking News, U.S. and World News". HuffPost (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2022-08-09.
- ↑ "idit harel caperton". be you. (kwa Kiingereza). 2013-04-09. Iliwekwa mnamo 2022-08-09.