Nenda kwa yaliyomo

Lango:Jiografia/Makala iliyochaguliwa/1

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
The printable version is no longer supported and may have rendering errors. Please update your browser bookmarks and please use the default browser print function instead.

Mabamba gandunia ya dunia yetu

Bamba gandunia ni kipande kikubwa cha ganda la dunia. Hoja la sayansi kuhusu gandunia ni ya kwamba ganda la dunia limevunjika kwa vipande mbalimbali vinavyoitwa mabamba. Kila bamba lapakana na mabamba mengine. Mabamba yasukumwa na mikondo ya moto chini yao kama majani yanayokaa usoni wa maji inayoanza kuchemka katika sufuria. Hivyo kila bamba lina mwendo wake wa pekee pamoja na au dhidi ya mabamba mengine.

Mabamba haya yote yameonekana kuwa na mwendo wa sentimita kadhaa (2 - 20 cm zimepimwa) kwa mwaka. Mwendo huu husababishwa na nguvu ya magma (mwamba moto wa kiowevu) inayopanda juu na kusukuma mabamba haya.