Msitu
Msitu ni mkusanyiko wa uoto asilia unaojumuisha miti ya aina mbalimbali, mimea na nyasi ambazo huweza kuwa fupi au ndefu.
Misitu inaweza kuwa ya asili au ya kupandwa na binadamu.
Mara nyingi wanyama mbalimbali, wakubwa kwa wadogo, huishi na hutegemea uoto huo kwa kuwatimizia mahitaji yao kwa malazi na chakula.
Hata hivyo maisha ya binadamu hutegemea mazingira yake yanayomzunguka katika kujikimu kwani kupitia misitu mvua hunyesha na hivyo kusababisha ustawi na ongezeko la chakula.
Ni kwamba asilimia kubwa ya watu hutegemea kilimo ili kujipatia mahitaji yao ya kila siku, hasa katika nchi za Afrika ambazo ziko nyuma sana katika nyanja za utumiaji wa teknolojia za kisasa kama utumiaji wa zana za kilimo, k.mf. matrekta.
Hivyo katika kutimiza upatikanaji wa chakula kwa wingi ni lazima misitu ilindwe kwa nguvu zote katika ukuaji na ustawi wa jamii.
Tunatakiwa tutunze misitu kwa ajili ya manufaa yetu wenyewe na vizazi vingine kwa sababu misitu inatusaidia kwa utalii na tunaweza kupata mvua. Njia za kufuata katika utunzaji wa misituː
- kupanda miti sehemu iliyokatwa miti
- kupunguza kilimo cha kuhamahama
- kuzuia uwindaji wa wanyama kwa kuchoma misitu
- kuzuia ongezeko la watu katika eneo dogo
- kuelimisha jamii juu ya utunzaji misitu
Faida za misitu ni:
- Husaidia katika mfumo wa mvua
- Hutumika kama makazi ya wanyama
- Ni chanzo cha mapato ya nchi
- Hutupatia dawa na chakula
Hasara za ukataji mitiː
- unasababisha mmomonyoko wa udongo
- unasababisha ukame
- unakaribisha jangwa
- unasababisha mvua za misimu
- uharibifu wa mazingira
- ongezeko la hali joto
Hivyo ni bora kutunza misitu kwa ajili ya manufaa yetu sisi na vizazi vijavyo. Ni muhimu kuwashauri watu watunze sana vyanzo vya asili kama misitu: hii ni kwa faida yetu wenyewe, inatusaidia hata kupata mvua kwa wingi.
pia kuhusu misitu tunajuakwamba kuna misitu ya asili na isiyo ya asili.Misitu ya asili ni misitu ambayo huota yenyewe bila kupandwa na mwanadamu.mfano msitu wa udzungwa(MLIMBA)
Misitu isiyo ya asili,ni misitu ambayo hupandwa na mwanadamu.kwahiyo mpaka hapo tumeshjua tofauti ya misitu ya asili na isiyo ya asili.
Makala hii kuhusu mambo ya biolojia bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Msitu kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |