Vitamini C
Vitamini C ni vitamini inayopatikana hasa katika matunda na majani mabichi. Kikemia ni aina ya asidi askobini na binadamu ni kati ya spishi chache ambazo haziwezi kutengeneza asidi hii mwilini. Kwa hiyi watu hutegemea chakula chenye kiwango cha vitamini hii.
Vitamini C ina kazhi muhimu katika mchakato wa kupona vidonda mwilini. Uhaba wake kwa muda mrefu unasababisha ugonjwa wa kiseyeseye (au hijabu). Kiseyeseye husababisha ufizi wa meno kuwa na vidonda na pia vidonda vingine mwilini kutopoa. Ugonjwa huu ulijulikana hasa wakati wa safari ndefu za baharini. Zamani haikujulikana chanzo chake kilikuwa nini; meli na jahazi zilibeba tu unga wa mkate au mchele kama chakula kilichoongezwa kwa nyama kavu au samaki kutoka baharini lakini matunda hayakuwa kawaida. Mabaharia wengi waligonjeka na kufa. Katika karne ya 19 mabaharia walitambua ya kwamba akiba ndogo ya malimau inaweza kuokoa watu kama wanakunjwa kijiko cha maji ya limau kila baada ya siku kadhaa.
Mwaka 1928 vitamini C iligundiuliwa pia kikemia na tangu 1928 ilithebitishwa kuwa inasmimamisha kiseyeseye.
Mahitaji ya mwili hukadiriwa kuwa miligramu 60-100 kwa siku; kiwango hiki kinapatikana kwa njia ya chakula cha kawaida.
Vyanzo
Matunda kama limau, chungwa na balungi ni vyanzo bora vya vitamini C. Kwa jumla karibu matunda yote yenye ladha ya kichungu ni chanzo chake.
Kuna pia aina za nyama na samaki zinazopeleka vitamini C mwilini. Hapo ndipo sababu ya kwamba Waeskimo hawakuwa na kiseyeseye ingawa zamani waliishi bila matunda kwa miezi mingi lakini walikula samaki bichi.
Kupika chakula kwa muda mrefu kunaharibu asidi ya vitamini C.
Matunda | mg vitamini C kwa kila gramu 100 za tunda | Matunda | mg vitamini C kwa kila gramu 100 za tunda | Matunda | mg vitamini C kwa kila gramu 100 za tunda |
---|---|---|---|---|---|
CamuCamu | 2800 | Limau | 40 | Mizabibu | 10 |
Rose hip | 2000 | Melon, cantaloupe | 40 | Apricot | 10 |
Acerola | 1600 | Cauliflower | 40 | Plum | 10 |
Jujube | 500 | Grapefruit | 30 | Watermelon | 10 |
Baobab | 400 | Raspberry | 30 | Ndizi | 9 |
Blackcurrant | 200 | Tangerine/ Mandarin oranges | 30 | Karoti | 9 |
Indian gooseberry | 445 | Passion fruit | 30 | Avocado | 8 |
Guava | 100 | ||||
Kiwifruit | 90 | Spinach | 30 | Crabapple | 8 |
Broccoli | 90 | Cabbage Raw green | 30 | Peach | 7 |
Loganberry | 80 | Lime | 20 | Tofah | 6 |
Redcurrant | 80 | Mango | 20 | Blackberry | 6 |
Brussels sprouts | 80 | Melon, honeydew | 20 | Beetroot | 5 |
Lychee | 70 | Raspberry | 20 | Pear | 4 |
Persimmon | 60 | nyanya | 10 | Lettuce | 4 |
Papaya | 60 | Blueberry | 10 | Cucumber | 3 |
Strawberry | 50 | mananasi | 10 | Fig | 2 |
Orange | 50 | Pawpaw | 10 | Bilberry | 1 |
Aina ya nyama | mg vitamini C kwa gramu 1000 za chakula | Aina ya nyama | mg vitamini C kwa gramu 1000 za chakula | Aina ya nyama | mg vitamini C kwa gramu 1000 za chakula |
---|---|---|---|---|---|
Ndama maini (bichi) | 36 | Kuku maini (fried ) | 13 | Mbuzi maziwa (bichi) | 2 |
ng’ombe maini (bichi) | 31 | Kondoo maini (ya kuchoma) | 12 | NYama ya ng’ombe nyekundu (ya kuchoma) | 0 |
Oysters (bichi) | 30 | Lamb heart (ya kuchoma) | 11 | Mayai ya kuku (bichi ) | 0 |
Cod Roe (ya kuchoma) | 26 | Kondoo ulimi (stewed) | 6 | Nyguruwe Bacon (ya kuchoma) | 0 |
Nguruwe maini (bichi) | 23 | Maziwa ya binadamu (bichi) | 4 | Nyama ya ndama (ya kuchoma) | 0 |
Lamb brain (ya kupikwa) | 17 | Cows maziwa (bichi) | 2 | Chicken leg (ya kuchoma) | 0 |