Isidori wa Sevilia
Isidori alizaliwa Cartagena (Hispania) mwaka 560 akafariki tarehe 4 Aprili 636 huko Sevilia alipokuwa askofu.
Anaheshimiwa kama mtakatifu, babu wa Kanisa na mwalimu wa Kanisa.
Ni msimamizi wa mtandao na wa wanafunzi.
Sikukuu yake inaadhimishwa kila tarehe 4 Aprili.
Maisha
Alizaliwa na Severianus na Turtura huko Cartagena (Hispania), akiwa wa nne kati ya watoto watano, ambao wanne kati yao wanaheshimiwa na Kanisa Katoliki kama watakatifu: Leandro wa Sevilia, Fulgensi, Fiorentina wa Cartagena naye mwenyewe.
Baada ya kuwa mkleri huko Sevilia, Isidori alimrithi kaka yake Leandro kama askofu wa jimbo kuu hilo.
Alishika nafasi ya maana katika matukio ya nchi yake wakati huo ilipotawaliwa na kabila la Kijerumani la Wavisigoti, ambao aliwavuta kutoka uzushi wa Ario kwenye imani ya Mtaguso wa kwanza wa Nisea na ya Mtaguso wa kwanza wa Konstantinopoli.
Pia alistawisha elimu yoyote na fasihi kuliko wote wa wakati wake.
Maandishi
Aliandika sana juu ya mambo mbalimbali: sayansi, historia, teolojia, maadili na ufafanuzi wa Biblia.
Vitabu muhimu zaidi ni vile 20 vya Etymologiae, ambavyo vilikusanya ujuzi wote wa wakati ule vikatumika sana katika Karne za Kati. Tafsiri yake ya kwanza kwa Kiingereza ni: Barney, Stephen A., Lewis, W. J., Beach, J. A. and Berghof, Oliver (translators). The Etymologies of Isidore of Seville. Cambridge: Cambridge University Press, 2006. ISBN 0521837499, ISBN 9780521837491.
Vyanzo
- Henderson, John. The Medieval World of Isidore of Seville: Truth from Words. Cambridge: Cambridge University Press, 2007. ISBN 0-521-86740-1.
- Herren, Michael. "On the Earliest Irish Acquaintance with Isidore of Seville." Visigothic Spain: New Approaches. James, Edward (ed). Oxford: Oxford University Press, 1980. ISBN 0-19-822543-1.
- Englisch, Brigitte. "Die Artes liberales im frühen Mittelalter." Stuttgart, 1994.
- Jones, Peter. "Patron saint of the internet", telegraph.co.uk., August 27, 2006 (Review of The Etymologies of Isidore of Seville, Cambridge University Press, 2006 (ISBN 0-521-83749-9)
- Shachtman, Noah. "Searchin' for the Surfer's Saint", wired.com., January 25, 2002
Viungo vya nje
- Baadhi ya maandishi yake kutoka The Latin Library
- Chronicon (katika tafsiri ya Kiingereza)
- The Etymologiae (complete Latin text)
- Henry Wace, Dictionary of Christian Biography, ccel.org
- Encyclopædia Britannica, 1911 edition: Isidore of Seville, 1911encyclopedia.org
- Order of St. Isidore of Seville, st-isidore.org