Nenda kwa yaliyomo

Augusto

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Pitio kulingana na tarehe 03:16, 28 Novemba 2011 na JhsBot (majadiliano | michango) (Robot: ko:아우구스투스 is a featured article)
Sanamu ya Kaisari Augusto

Augusto alikuwa Kaisari wa kwanza wa Dola la Roma kuanzia mwaka 27 KK hadi 14 BK. Jina lake la kiraia lilikuwa Gaius Octavius akizaliwa Italia tarehe 23 Septemba 63 KK. Octavius alikuwa mpwa wa Julius Caesar aliyempenda kijana na kumteua kama mrithi katika agano lake.

Historia ya Augusto ina vipindi viwili:

  • kipindi cha kwanza kinamwonyesha mwanasiasa kijana ambaye ni mkali akitafuta kulipiza kisasi mauaji wa mjomba wake na kushinda maadui wote katika vita ya wenyewe kwa wenyewe.
  • kipindi cha pili kinamwonyesha mtawala wa Dola la Roma mwenye upole na hekima anayefaulu kujenga Roma upya katika kipindi kirefu cha amani na maendeleo

Majina

Augusto anajulikana kwa majina mbalimbali.

  • alizaliwa kama Gaius Octavius
  • baada ya kusilikiwa na Caesar alitumia jina lake
  • Hivyo aliitwa Gaius Iulius Caesar Octavianus yaani "Julius Caesar wa familia ya Octavius"
  • tangu 31 KK alitumia pia cheo "Imperator" (mwenye amri, "amiri") kama jina la kwanza
  • 27 KK alipewa jina la heshima la "Augustus" aliitwa "Imperator Caesar Augustus"
Kifo cha Caesar (taswira ya 1867) - Tar. 15 Machi 44 KK Julius Caesar aliuawa na Marcus Junius Brutus na Gaius Cassius Longinus.

Mrithi wa Caesar

Alikuwa kijana wa miaka 19 aliyejiandaa kuwa afisa wa jeshi kwa mara ya kwanza katika maisha yake aliposikia habari za kuuawa kwa Julius Caesar. Alikimbia Roma mara moja alipopata habari ya kuwa Caesar alimsiliki na kumtaja kama mritji katika agano. Hapa aliamua kulipiza kisasi wauaji wa Caesar hivyo akaingia katika siasa ya Roma na kipindi cha vita ya wenyewe kwa wenyewe kilichofuata mauaji ya kiongozi wa dola.

Kushindana na kupatana na Marcus Antonius

Rafiki yake marehemu Marcus Antonius hakukubali agano akatwaa mali yote lakini watu wengi na wanajeshi wa Caesar walisimama upande wa Octavius. Huyu aliajiri askari na kujenga jeshi na mwaka 43 alitwaa mji wa Roma kwa nguvu ya kijeshi wakati Marcus Antonius alikuwa mbali huko Gallia. Senati ya Roma ilikubali hatua hii na kumchagua kuwa seneta. Aliendelea kuongoza jeshi la Senati na kumshinda Marcus Antonius kwenye mapigano huko Italia ya Kaskazini.

Konsuli wa Roma na mtawala katika ushirikiano

Baada ya ushindi huu alikubaliwa kama konsuli wa Roma akaendelea kupatana na Marcus Antonius na kujenga ushirikiano naye. Pamoja walitawala Roma baafa ya kupewa madaraka ya kidikteta na senati kwa muda wa miaka 5 na baadaye miaka 5 tena.

Mwaka 42 walifaulu kuwashinda wauaji wa Caesar waliokaa Ugiriki na baadaye waligawana eneo la dola kati yao; Octavianus alikuwa mkuu wa sehemu ya magharibi na Marcus Antonius mkuu wa sehemu za mashariki alipomwoa Kleopatra malkia wa Misri.

Mapigano ya baharini ya Aktium' ya 31 KK' (taswira ya 1672)
Dola la Roma baada ya Augusto
kijani nyeusi: Majimbo chini ya Roma
kijani nyeupe: maeneo lindwa chini ya Roma yenye kiwango cha kujitawala;
kijani nyeupe nje ya mstari mweusi: Jimbo la Germania Magna lililopotea baada ya mwaka 9

Ushindi juu ya Marcius Antonius

Maelewano kati yao yalizorota na mwaka 33 walitengana. Octavianus alimshinda Marcus katika mapigano ya baharini ya Aktium tar. 2 Septemba 31 KK na huyu alijiua pamoja na Kleopatra. Baada ya kuvamia na kuteka Misri Octavianus alirudi Roma mjini mwaka 29 KK akawa mtawala wa pekee.

Mtu wa kwanza

Hapa Roma alishangaza watu wote akirudisha mamlaka yake ya kidikteta kwa senati. Aliombwa kuendelea kama mkuu wa jeshi akakubali. Alikataa kupokea madaraka ya dikteta kwa muda wa maisha yake.

Kwa njia hiyo alirudisha katiba ya jamhuri iliyotawaliwa na senati na maafisa yake. Lakini hali halisi alishika mamlaka yote kama mtawala mkuu aliyeheshimu taasisi za jamhuri. Ni hekima hii iliyosifiwa na wengi ya kuwa hakuendlea kujipatia cheo cha mfalme au cha dikteta akaridhika kuitwa raia wa kwanza.

Utwala wake ulileta kipindi kirefu cha amani ya ndani. Wananchi walioteseka na miaka ya vita ya wenyewe kwa wenyewe waliweza kujenga maisha upya na uchumi ulistawi.

Milki kubwa ya Misri ilikuwa sehemu ya Dola la Roma. Hata sehemu nyingi za Germania ziliingizwa katika dola. Vita ya pekee iliyoenda vibaya ilikuwa jaribio la kupanusha mipaka ya Roma katika Germania hadi mto Elbe. Wagermania waliangamiza legioni tatu na mpaka wa Kiroma ulirudishwa hadi mto Rhine.

WikiMedia Commons
WikiMedia Commons
Wikimedia Commons ina media kuhusu:


Makala hii kuhusu Kaizari fulani wa Roma bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Augusto kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.

Kigezo:Link FA Kigezo:Link FA Kigezo:Link FA Kigezo:Link FA Kigezo:Link FA Kigezo:Link FA Kigezo:Link FA Kigezo:Link FA Kigezo:Link FA Kigezo:Link FA Kigezo:Link FA Kigezo:Link FA Kigezo:Link FA Kigezo:Link FA