Nenda kwa yaliyomo

Oppland

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Pitio kulingana na tarehe 19:06, 1 Agosti 2011 na Muddyb (majadiliano | michango) (Ukurasa ulianzishwa kwa kuandika ''''Oppland''' ni moja kati ya Majimbo ya Norwei. Jimbo limepakana na Sør-Trøndelag, Møre og Romsdal, Sogn og Fjordane, Buskerud, [[Akershus]...')
(tofauti) ← Pitio lililotangulia | Toleo la sasa (tofauti) | Pitio linalofuata → (tofauti)

Oppland ni moja kati ya Majimbo ya Norwei. Jimbo limepakana na Sør-Trøndelag, Møre og Romsdal, Sogn og Fjordane, Buskerud, Akershus, Oslo na Hedmark. Ngazi ya utawala ya jimboni hapani ipo mjini Lillehammer. Oppland pamoja na Hedmark, ni moja kati ya majimbo pekee yaliyozungukwa na bandari nchini Norwei.

Jiografia

Oppland imeenea kutoka maziwa Mjøsa na Randsfjorden hadi kuelekea katika milima ya Dovrefjell, Jotunheimen na Rondane. Jimbo hili limegawanyika katika wilaya za zamani. Ambazo ni Gudbrandsdalen, Valdres, Toten, Hadeland na Land.

Oppland ukubwa wake unamujumuisha miji ya Lillehammer, Gjøvik, Otta na Fagernes, na milima miwili mirefu sana ya Norwei, ambayo ni Glittertind na Galdhøpiggen.

Kuna majumba ya makumbusho kadhaa na vivutio vingine vilivyopo mjini Oppland na utalii ni pato muhimu sana kwa uchumi, Valdres na Gudbrandsdal huwa miongoni mwa vivutio mashuhuri sana. Gudbrandsdal imezunguka mto Gudbrandsdalslågen, na ina vijiji kama vile Øyer, Dovre na Dombås. Valdres inajumuisha eneo linaloanzia kutoka Jotunheimen hadi Bagn katika mto Begna. Ni sehemu mashuhuri sana kwa mchezo wa skiing na michezo mingine ya kipindi cha baridi. Mahali ambapo kuna wakazi wengi katika jimbo hili ni Beitostølen na Fagernes.

Manispaa

Mahali pa Manispaa za Oppland
Mahali pa Manispaa za Oppland

Jimbo la Oppland lina jumla ya manispaa 26:

  1. Dovre
  2. Etnedal
  3. Gausdal
  4. Gjøvik
  5. Gran
  6. Jevnaker
  7. Lesja
  8. Lillehammer
  9. Lom
  10. Lunner
  11. Nord-Aurdal
  12. Nord-Fron
  13. Nordre Land
  1. Østre Toten
  2. Øyer
  3. Øystre Slidre
  4. Ringebu
  5. Sel
  6. Skjåk
  7. Søndre Land
  8. Sør-Aurdal
  9. Sør-Fron
  10. Vågå
  11. Vang
  12. Vestre Slidre
  13. Vestre Toten

Viungo vya Nje

Marejeo


{{mbegu-jio-Norwei]]