Nenda kwa yaliyomo

Baden-Württemberg

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Pitio kulingana na tarehe 15:52, 23 Agosti 2010 na Xqbot (majadiliano | michango) (roboti Nyongeza: sc:Baden-Württemberg)
Mahali pa Baden-Württemberg katika Ujerumani

Baden-Württemberg ni moja ya majimbo 16 ya kujitawala ya Ujerumani lenye wakazi milioni 10.7 kwenye eneo la 35 752 km². Mji mkuu ni Stuttgart. Waziri mkuu ni Stefan Mappus (CDU). Jimbo liko katika kusini magharibi ya nchi likipakana na Ufaransa na Uswisi.

Historia

Baden-Württemberg imeanzishwa 1952 baada ya vita kuu ya pili ya dunia kutokana na majimbo ya kihistoria ya Baden, Württemberg na Hohenzollern. Yaliungana baada ya kura ya wananchi wote.

Historia ya kuandikwa ilianza miaka 2,000 iliyopita wakati sehemu kubwa ya jimbo lilikuwa sehemu ya Dola la Roma. Chanzo cha miji mingi ni mji wa Kiroma au kambi la jeshi la Roma.

Boma la Heidelberg

Jiografia

Jimbo lapakana na Uswisi upande wa kusini, Ufaransa upande wa magharibi na majimbo ya Kijerumani ya Rhine-Palatino, Hesse na Bavaria.

Miji mikubwa ni pamoja na Stuttgart, Mannheim, Karlsruhe, Freiburg, Heidelberg, Heilbronn, Ludwigsburg, Ulm, Tübingen, Pforzheim na Reutlingen.

Bonde la mto Rhine pamoja na ziwa la Konstanz ni mpaka wa kusini na magharibi. Kuna safu mbili za milima ya Msitu Mweusi na Safu ya Swabonia.

Rhine, Neckar na Danubi ni mito muhimu zaidi.

Hali ya hewa hutegemea na mahali kama ni mlimani au bondeni. Mabonde ya Baden-Württemberg hasa bonde la Rhine yaona halijoto ya juu kulingana na maeneo mengine ya Ujerumani. Hii ni sababu muhimu kwa kilimo cha mizabibu na sifa nzuri ya divai la jimbo

Jengo la Mercedes-Benz-Center Stuttgart

Uchumi

Jimbo lasifiwa kwa ubuni za kiteknolojia. Idadi ya watu wanaoandikisha ubuni mpya ni kubwa kulingana na majimbo mengine yote ya Ujerumani. Sifa hii imesababisha jimbo kuwa na uchumi imara kushinda penginepo. Mapato ni makubwa na idadi ya watu wasio na ajira ni ndogo. Kuna makampuni mengi madogo na ya wastani yanayouza bidhaa zao kote Ulaya na kimataifa.

Kati ya makampuni makubwa ni hasa Daimler watengenezaji y magari aina Mercedes-Benz.

Utamaduni

Baden-Württemberg imetunza desturi nyingi. Lahaja za Kijerumani ni tofauti-tofauti katika wilaya mbalimbali. Chakula na divai ina tabia za pekee.

Kwa wenyeji tofauti kati ya "Swabia" na "Baden" ni muhimu - kwa jumla tofauti kati ya watu wa bonde la Rhine na wale wa milimani.

Historia imeacha magofu mengi ya maboma ya makabaila waliotawala maeneo madogo-madogo.

Picha za Baden-Württemberg

Tovuti za Nje

WikiMedia Commons
WikiMedia Commons


Makala hii kuhusu maeneo ya Ujerumani bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Baden-Württemberg kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.


 
Majimbo ya Ujerumani
Baden-WürttembergBavaria (Bayern)BerlinBrandenburgBremenHamburgHesse (Hessen)Mecklenburg-Pomerini Magharibi (Mecklenburg-Vorpommern)Saksonia Chini (Niedersachsen)Rhine Kaskazini-Westfalia (Nordrhein-Westfalen)Rhine-Palatino (Rheinland-Pfalz)Saar (Saarland)Saksonia (Sachsen)Saksonia-Anhalt (Sachsen-Anhalt)Schleswig-HolsteinThuringia (Thüringen)