Nenda kwa yaliyomo

Bata-miti

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Pitio kulingana na tarehe 10:47, 28 Septemba 2009 na TXiKiBoT (majadiliano | michango) (roboti Nyongeza: br:Dendrocygna)
Bata-miti
Bata-miti uso-mweupe
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Chordata (Wanyama wenye ugwe wa neva mgongoni)
Ngeli: Aves (Ndege)
Oda: Anseriformes (Ndege kama bata)
Familia: Anatidae (Ndege walio na mnasaba na bata)
Jenasi: Dendrocygna Swainson, 1837

Mabata-miti au Dendrocygninae ni familia ndogo ya familia ya Anatidae yenye jenasi moja tu, Dendrocygna. Waainishaji wengine wanawaweka ndani ya familia yao wenyewe Dendrocygnidae au ndani ya kabila Dendrocygnini ya familia ndogo Anserinae. Leo kuna spishi nane za mabata-miti na visukuku vya spishi ingine vimefunuliwa kisiwani kwa Aitutaki, Visiwa vya Cook. Wanaitwa mabata-miti kwa sababu hujenga matago yao pengine ndani ya miti. Lakini kwa Kiingereza wanaitwa “whistling ducks” sikuhizi kwa sababu ya sauti yao kama mluzi. Mabata hawa wanatokea popote kwa kanda za tropiki na nusu-tropiki. Wana miguu mirefu na shingo refu na wanapenda kuwa pamoja. Makundi makubwa ya ndege hawa huonekana maziwani.

Spishi za Afrika

Spishi za mabara mengine

Picha