Nenda kwa yaliyomo

Max Weber

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Pitio kulingana na tarehe 17:32, 28 Mei 2009 na Xqbot (majadiliano | michango) (roboti Nyongeza: gan:韋伯; cosmetic changes)
Max Weber mnamo 1894

Maximilian Carl Emil Weber (21 Aprili 186414 Juni 1920) alikuwa mwanasheria na mtaalamu wa siasa na sayansi ya jamii nchini Ujerumani.

Maisha

Alisoma sheria, uchumi, falsafa na historia kwenye vyuo vikuu vya Heidelberg, Berlin na Göttingen. Mwaka 1889 alichukua cheo cha dokta wa sheria kwenye chuo kikuu cha Berlin. Akaendelea kuwa profesa wa uchumi huko Freiburg na tangu 1897 kwenye chuo kikuu cha Heidelberg. 1889 aliondoka kwenye chuo kikuu kutokana na ugonjwa akaendelea kuhariri gazeti la sosiolojia na kuandika vitabu.

Baada ya vita kuu ya kwanza ya dunia alikuwa mshauri wa serikali ya Ujerumani kwenye majadiliano kwa mkataba wa Versailles na ndani ya Ujerumani alikuwa kati ya waanzilishaji wa chama huria cha demokrasia. 1919 alianza kufundisha tena kwenye chuo kikuu lakini 1920 alikufa.

Kazi

Weber aliandika mengi kuhusu uchumi, utawala, siasa na dini. Kati ya maandiko yaliyokuwa mashuhuri hasa ni "Maadili ya kiprotestanti na roho ya ubepari" (Die protestantische Ethik und der 'Geist' des Kapitalismus). Hapa alitoa hoja ya kuwa roho ya uprotestanti ilisababisha wafuasi wake kubana matumizi ya fedha kwa maisha tajiri na kuridhika maisha ya wastani hata kama wamefaulu kiuchumi. Maadili haya yaliwawezesha kukusanya rasilmali iliyokuwa msingi muhimu kwa mapinduzi ya viwandani.


Viungo vya Nje

Maandiko ya Weber:

Kuhusu Weber:

Kigezo:Link FA Kigezo:Link FA Kigezo:Link FA